Sunday 7 March 2010

Owen nje msimu wote, Hargreaves kurudi dimbani!!
Mshambuliaji wa Manchester United Michael Owen hatacheza tena msimu huu baada ya kuumia musuli za mguu katika Fainali ya Kombe la Carling walipoifunga Aston Villa 2-1.
Owen, miaka 30, ndie aliifungia Man United bao la kwanza katika Fainali hiyo na ikabidi atoke Kipindi cha Kwanza baada ya kuumia.
Sasa imefahamika maumivu hayo yatalazimika kufanyiwa opersheni na hilo litamweka nje hadi msimu unakwisha.
Nae majeruhi wa muda mrefu Owen Hargreaves ataonekana uwanjani siku ya Alhamisi akicheza mechi ya Timu ya Pili ya Manchester United itakapopambana na Kikosi cha pili cha Manchester City.
Hargreaves hajacheza tangu Septemba 2008 na alifanyiwa operesheni kwenye magoti yake mawili huko Marekani.
LA LIGA: Real watwaa uongozi!!
Baada ya Barcelona kutoka sare ya 2-2 na Almeria hapo jana, Real Madrid waliokuwa nyuma kwa bao 2-0 walipocheza na Sevilla, waliibuka na kupata ushindi wa mabao 3-2 na hivyo kutwaa uongozi wa La Liga.
Sevilla walipata bao la kwanza baada ya Xabi Alonso kujifunga mwenyewe na Dragutinovic kufunga la pili kwa frikiki.
Lakini Real wakajitutumua na kufunga kupitia Ronaldo, Ramos na Van de Vaart na hivyo kufungana pointi 62 na Barcelona lakini Real wana magoli bora.

No comments:

Powered By Blogger