Thursday 11 March 2010

UEFA CHAMPIONS LIGI: Real waikosa Fainali kwao, watoswa na Lyon!
Man United 4 AC Milan 0
Wayne Rooney alichomeka bao 2, Park na Fletcher wakapiga moja moja na kuishindilia AC Milan misumari minne na kuiingiza Manchester United Robo Fainali lakini kilio kikubwa kilitokea Uwanja wa Bernabeau baada ya Real Madrid kutolewa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI huku Mei 22 Fainali ikitakiwa ichezwa Uwanja huo huo wa Bernabeau.
Alikuwa Mchezaji wa zamani wa Manchester United Cristiano Ronaldo aliewapa matumaini Real alipofunga goli dakika ya 5 na kufanya Timu hizo zifungane kwa bao 1-1 kwani Lyon walishinda 1-0 mechi ya kwanza.
Alieleta msiba mkubwa Hispania ni Miralem Pjanic aliposawazisha dakika ya 75 na hivyo kuipa Lyon ushindi wa jumla ya bao 2-1.
Mbali ya kutegemea kucheza Fainali Uwanja wa nyumbani hii ni mara ya 6 mfululizo Real Madrid wanabwagwa nje ya Mashindano haya kwenye hatua hii na hili ni pigo kubwa sana kwa Klabu iliyonunua Masupastaa kwa bei mbovu.

No comments:

Powered By Blogger