Sunday 7 March 2010

KWA UFUPI TU:
Allardyce ampaka Rafa!
Bosi wa Blackburn Sam Allardyce amejibu mapigo kwa Bosi wa
Liverpool Rafa Benitez katika vita yao ya maneno iliyoanza muda mrefu na kupamba moto baada ya Liverpool kuifunga Blackburn bao 2-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu wikiendi iliyokwisha.
Tangu Benitez atue England mwaka 2004 amekuwa hana uhusiano mzuri na Allardyce na kila Timu zinazoongozwa na Mameneja hao zikikutana malumbano makali hutokea kati yao.
Mara baada ya mechi ya wikiendi iliyopita, Benitez alidai Blackburn walikuwa wakitumia miguvu na pasi ndefu tu.
Allardyce amejibu: “Yeye anajua Timu yake ilicheza mpira mbovu na ni bahati tu walishinda! Anajaribu kunilaumu mimi ili akwepe lawama za ubovu wa Liverpool!”
Kuszczak: “Nipeni namba au naondoka!”
Kipa wa akiba wa Manchester United Tomasz Kuszczak ambae yuko msimu wake wa nne Klabuni hapo ametaka awe anapewa namba au ataondoka mwishoni mwa msimu huu.
Kuszczak, miaka 27, ni Kipa nambari mbili nyuma ya Edwin van der Sar, miaka39, ambae ameongeza mkataba wake na Manchester United hadi mwishoni mwa msimu wa 2011.

No comments:

Powered By Blogger