Wednesday 10 March 2010

UEFA CHAMPIONS LIGI: Arsenal, Bayern zatinga Robo Fainali!!
• Arsenal 5 FC Porto 0
• Fiorentina 3 Bayern Munich 2

Mabao matatu ya Niklas Bendtner na moja moja la Nasri na Eboue yameiangamiza FC Porto kwa bao 5-0 na hivyo kuupindua ushindi wa FC Porto wa bao 2-1 katika mechi ya kwanza na kuipeleka Arsenal Robo Fainali kwa jumla ya bao 6-2.
Mabao ya Arsenal yalifungwa dakika ya 10 na ya 25 na Bendtner.

Kipindi cha pili Nasri alifunga bao ya dakika 63 na Eboue dakika ya 66 na Bendtner akamalizia kwa penalti dakika ya 90.
Huko Italia, licha ya Bayern Munich kupigwa 3-2 na Fiorentina imetinga Robo Fainali kwa mabao ya ugenini.
Bayern Munich ilishinda mechi ya kwanza 2-1 na hivyo kuyafanya jumla ya magoli baada ya mechi mbili kuwa 4-4 na hivyo sheria ya goli la ugenini kutumika.
UEFA CHAMPIONS LIGI: Mechi za marudiano
RATIBA:
Jumatano, 10 Machi 2010
Man United v AC Milan
Real Madrid v Lyon
MATOKEO MECHI ZA KWANZA:

AC Milan 2 v Man United 3
Lyon 1 v Real Madrid 0

1 comment:

Shelly said...

NAONA USHINDI UKIWA SI WA MAN U, HUZAMI SANA KWENYE UCHAMBUZI. TUNANGOJA MBWEMBWE ZAKO BAADA YA MECHI YA MAN U NA MILAN. PAMOJA NA KUKUKOSOWA KIBINADAMU, NAPONGEZA KAZI YAKO. UKO JUU MTU WANGU

Powered By Blogger