Friday 12 March 2010

EUROPA LIGI: Liverpool, Fulham zapigwa ugenini!!
Klabu za England, Liverpool na Fulham, jana zilipoteza mechi zao za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za ugenini.
Liverpool ilifungwa 1-0 na Lille huko Ufaransa na Fulham ilitwangwa 3-1 na Juventus huko Italia.
Bao lililoiua Liverpool lilifungwa dakika ya 85 na Mchezaji wa Lille Eden Hazard.
Huko Italia, Juventus ilifunga bao zake 3 kipindi cha kwanza kupitia Nicola Legrottaglie, Jonathan Zebina na David Trezeguet.
Bao la Fulham lilifungwa na Dickson Etuhu.
Timu hizo zitarudiana wiki ijayo Machi 18.
Matokeo kamili:
Atletico Madrid 0 v Sporting Lisbon 0
Benfica 1 v Marseille 1
Hamburg 3 v Anderlecht 1
Juventus 3 v Fulham 1
Lille 1 v Liverpool 0
Panathinaikos 1 v Standard Liege 3
Rubin Kazan 1 v Wolfsburg 1
Valencia 1 v Werder Bremen 1
DROGBA NI BORA AFRIKA
Mchezaji kutoka Ivory Coast na anaechezea Klabu ya Chelsea, Didier Drogba, miaka 32, amechukua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika na kuwapiku Michael Essien na Samuel Et’oo.
Drogba aliwahi kuchukua Tuzo hii mwaka 2006.
Algeria ilishinda Tuzo ya Timu Bora Afrika.
Magazeti Italia yalia: “NI FEDHEHA!”
Kufuatia vipigo vya nje ndani, 3-2 wakiwa kwao San Siro na 4-0 ndani ya Old Trafford , Magazeti ya Italia yameweka Mabango makubwa yakilalamika kuhusu kipigo cha 4-0 cha Jumatano cha AC Milan mikononi mwa Manchester United kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI huko Old Trafford.
Gazeti moja kubwa lilitamka: “Hapo zamani za kale, ilikuwepo Milan!” wakimaanisha enzi za AC Milan waliponyakua Ubingwa wa Ulaya mara 7.
Jingine lilisema: “Milan yaadhiriwa! Somo toka kwa Rooney! Si kushindwa ni kipondo!”
Gazeti moja liliandika kuwa kufungwa na Manchester United kunakubalika lakini jinsi walivyopigwa 4-0 bila ya Timu kuonyesha uchungu wowote ndilo linauma sana.
LIGI KUU England: RATIBA WIKIENDI HII:
[saa za bongo]
Jumamosi, Machi 13
[saa 9 dak 45 mchana]
Tottenham v Blackburn
[saa 12 jioni]
Birmingham v Everton
Bolton v wigan
Burnley v Wolves
Chelsea v West Ham
Stoke v Aston Villa
[saa 2 na nusu usiku]
Hull v Arsenal
Jumapili, Machi 14
[saa 10 na nusu jioni]
Man United v Fulham
[saa 1 usiku]
Sunderland v Man City
Jumatatu, Machi 15
[saa 5 usiku]
Liverpool v Portsmouth
Jumanne, Machi 16
[saa 4 dak 45 usiku]
Wigan v Aston Villa

No comments:

Powered By Blogger