Thursday 11 March 2010

LEO EUROPA LIGI: Liverpool wapo Ufaransa, Fulham ni Italia!
Timu za England, Liverpool na Fulham, leo zipo ugenini kwenye mechi za kwanza za EUROPA LIGI ambayo marudio yake ni wiki ijayo.
Hii ni hatua ya Mtoano ya Timu 16 na Liverpool wako Ufaransa kucheza na Lille wakati Fulham wako Italia kupambana na vigogo wa huko Juventus.
Mechi nyingine yenye mvuto ni ile ya majirani wa Spain na Ureno kati ya Atletico Madrid v Sporting Lisbon.
RATIBA:
Atletico Madrid v Sporting Lisbon
Benfica v Marseille
Hamburg v Anderlecht
Juventus v Fulham
Lille v Liverpool
Panathinaikos v Standard Liege
Rubin Kazan v Wolfsburg
Valencia v Werder Bremen
Fergie ampa changamoto Rooney
• Beckham, Kocha AC Milan wakiri Rooney ni bora duniani!
• Beckham akana kuwa nae ni Kijani na Dhahabu!!
Sir Alex Ferguson amemtaka Wayne Rooney aivunje rekodi aliyoweka Cristiano Ronaldo ya kufunga goli 42 kwa msimu aliyoiweka mwaka 2007-08.
Mpaka sasa Rooney ana jumla ya mabao 30 lakini mwenyewe amesema yeye hajaweka lengo lolote ila anachotaka ni magoli tu.
Rooney akizungumza baada ya jana kuipiga AC Milan bao 4-0 huku bao mbili zikifungwa na yeye, alisema: “Ni matokeo mazuri kwetu! “
Nae David Beckham, aliewahi kuichezea Manchester United na kisha kuhamia Real Madrid na baadae LA Galaxy na sasa yuko kwa mkopo AC Milan, alikiri Rooney ni kiboko kwa kusema: “Bila shaka, yeye ni kipaji na ni bora duniani pamoja na Ronaldo na Messi!
Na Kocha wa AC Milan Leonardo amekubali Timu yake ilizidiwa kila kitu na Manchester United na kusema Man United walicheza kandanda la hali ya juu.
Wakati huo huo David Beckham amekanusha kuwa na yeye anawapinga Wamiliki wa Manchester United Familia ya Glazer baada ya kuonekana mwishoni mwa mechi hiyo ya Manchester United v AC Milan akivaa skafu ya Kijani na Dhahabu aliyorushiwa na shabiki mmoja anaeunga mkono upinzani dhidi ya kina Glazer.
Rangi hizo za Kijani na Dhahabu ni rangi za Klabu anzilishi ya Man United, Newton Heath, na zimechukuliwa kama ishara ya upinzani.
Beckham amesema: “Mimi ni Shabiki wa Manchester United. Nilirushiwa ile skafu nikaivaa shingoni. Hizo ni rangi za zamani za Man United. Mimi naisapoti Klabu.”

No comments:

Powered By Blogger