Tuesday 9 March 2010

UEFA CHAMPIONS LIGI: Mechi za marudiano
RATIBA:
Jumanne, 9 Machi 2010
Arsenal v FC Porto
Fiorentina v Bayern Munich
Jumatano, 10 Machi 2010
Man United v AC Milan
Real Madrid v Lyon
Jumanne, 16 Machi 2010
Chelsea v Inter Milan
Sevilla v CSKA Moscow
Jumatano, 17 Machi 2010
Barcelona v VfB Stuttgart
Bordeaux v Olympiakos
MATOKEO MECHI ZA KWANZA:
AC Milan 2 v Man United 3
Lyon 1 v Real Madrid 0
Bayern Munich 2 v Fiorentina 1
FC Porto 2 v Arsenal 1
Olympiakos 0 v Bordeaux 1
VfB Stuttgart 1 v Barcelona 1
CSKA Moscow 1 v Sevilla 1
Inter Milan 2 v Chelsea 1
TATHMINI:
Arsenal v FC Porto
Cesc Fabregas, Nahodha wa Arsenal, ataikosa mechi muhimu ya marudiano na FC Porto ambayo Arsenal wanatakiwa washinde 1-0 ili wasonge mbele, kwa vile ni majeruhi.
Katika mechi ya kwanza, FC Porto ilishinda 2-1.
Mbali ya kumkosa Fabregas, Arsenal pia itamkosa Difenda William Gallas lakini
nafasi ya Gallas inategemewa kuzibwa na Sol Campbell na akikosekana yupo Mikel Sylvestre.
Nao FC Porto wamesema wao hawatui Uwanja wa Emirates ili kucheza kwa kujihami kulinda ushindi wao wa mechi ya kwanza wa 2-1 bali watashambulia tu kama staili yao ilivyo kila siku.
Chapombe Adriano!!
Mkurugenzi wa Klabu ya Flamengo Marcos Braz amesema Adriano amekumbwa na matatizo binafsi na ameanza tena kunywa pombe kwa wingi na mfululizo.
Braz amelalama: “Akianza kunywa, haachi! Alilishinda tatizo hili lakini limerudi tena kwa sababu ya presha ya matatizo binafsi!”
Braz amezipinga habari za Magazeti ya Brazil kuwa Adriano anatumia madawa ya kulevya.
Mwaka jana Adriano aliikimbia Inter Milan na kurudi kwao Brazil akidai kuwa hana furaha na ni mpweke huko Italia.
Adriano yupo kwenye Kikosi cha Brazil na anategemewa pia kuwemo kwenye Kikosi hicho kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Ameshaichezea Brazil mara 48 na kufunga magoli 27.
LIGI KUU: Liverpool yakong’otwa!
Kwenye mechi pekee ya Ligi Kuu hapo jana, Wigan imeifunga Liverpool bao 1-0 Uwanjani DW na hivyo kuitia kiwewe cha kuikosa nafasi ya 4 itakayowawezesha kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI msimu ujao.
Bao la ushindi la Wigan lilifungwa dakika ya 35 na Mshambuliaji Hugo Rodallega.
Baada ya mechi, Kocha wa Liverpool Rafa Benitez aliwalaumu Wachezaji wake kwa kutocheza vizuri na kupoteza pasi nyingi. Lawama hizo pia zilimlenga Straika wake Dirk Kuyt kwa kufanya kosa lililozaa goli lililowakata ngebe Liverpool.
Katika msimamo wa ligi, Liverpool wapo nafasi ya 6 wakiwa wamecheza mechi 29 na wana pointi 48 na mbele yao wapo Tottenham na Manchester City wote wakiwa na pointi 49 lakini Man City wamecheza mechi moja pungufu.
Nyuma ya Liverpool wapo Aston Villa waliocheza mechi 26 tu na wana pointi 45.

No comments:

Powered By Blogger