Wednesday 10 March 2010

UEFA CHAMPIONS LIGI: Leo ni kimbembe Old Trafford na huko Bernabeau!!
• Ni Man U v AC Milan na Real v Lyon
Baada ya Manchester United kuishindilia AC Milan 3-2 wakiwa kwao San Siro na Real Madrid kupigwa kimoja na Lyon huko Ufaransa, leo ni mechi za marudiano na leo Real wako kwao Uwanja wa Bernabeau kuikaribisha Lyon na Man United wako nyumbani Old Trafford.
Kwa Real Madrid, licha ya kuwa kwao, hii ni mechi muhimu mno sana hasa kwa vile Fainali ya Kombe hili la UEFA CHAMPIONS LIGI msimu huu itachezwa hapo hapo Bernabeau mwezi Mei na hivyo kila Mshabiki wao anajua kuwa wanawajibika kuweko kwenye Fainali hiyo na ni lazima leo waifunge Lyon ili ndoto yao kucheza Fainali hiyo Bernabeau ikamilike.
Huko Old Trafford, kwa Mashabiki wa Manchester United ni kumwona tena kipenzi chao cha zamani lakini safari hii ni ‘adui’ na huyo ni David Beckham akiwa na Timu yake ya mkopo AC Milan.
Ili waibwage Manchester United, AC Milan lazima waifunge bao 2-0 au upatikane ushindi bora zaidi ya ule wa Man United wa 3-2 ukizingatia magoli ya ugenini.
Kwa ufupi, mechi za leo ni kimbembe!!

No comments:

Powered By Blogger