Thursday 30 July 2009

AUDI CUP: Fainali Bayern v Man U!!
Bayern yaitandika AC Milan 4-1!!
Wenyeji Bayern Munich wakicheza Uwanja wa nyumbani Allianz Arena mjini Munich jana waliikung’uta AC Milan mabao 4-1 na leo watakutana na Manchester United kwenye Fainali ya Kombe la Audi.
Man U jana waliitoa Boca Juniors bao 2-1.
AC Milan leo watacheza na Boca kutafuta mshindi wa tatu.
Mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Thomas Muller, bao 2, Schweinsteger na Sene bao 1.

Bao la AC Milan lilipachikwa na Andreas Pirlo.
MATOKEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MECHI ZA MCHUJO JANA:
Apoel Nicosia 2 v Partizan Belgrade 0,
Celtic 0 v Dinamo Moscow 1,
FC Copenhagen 3 v Stabaek 1,
FC Levadia Tallinn 0 v Debreceni VSC 1,
FC Sheriff Tiraspol 0 v Slavia Prague 0,
FC Zurich 2 v NK Maribor 3,
FK Ventspils 1 v BATE Borisov 0,
Shakhtar Donetsk 2 v FCU Politehnica Timisoara 2,
Slovan Bratislava 0 v Olympiacos 2,
Sporting 0 v FC Twente 0,
MECHI YA KIRAFIKI:
Hannover 0 Arsenal 1
Obafemi Martins kwenda Wolfsburg?
Habari ambazo hazijathibitishwa na Newcastle zimesema Mshambuliaji kutoka Nigeria Obafemi Martins yuko mbioni kuihama Timu hiyo iliyoporomoka Daraja kutoka Ligi Kuu na kujiunga na Mabingwa wa Ujerumani Klabu ya Wolfsburg.
Imeelezwa Newcastle wameikubali ofa ya Wolfsburg ya Pauni Milioni 9.

No comments:

Powered By Blogger