Sunday 26 July 2009

Terry kubaki Chelsea!!
Nahodha wa Chelsea na England, John Terry, amewakata maini Manchester City kwa kuibuka na kutamka waziwazi kuwa yeye anabaki Chelsea.
Wiki za hivi karibuni kumekuwa na mazungumzo mazito kwamba Terry atakwenda Man City kwa kitita cha zaidi ya Pauni Milioni 40 habari zilizopamba moto hasa kutokana na ukimya wa Terry mwenyewe ingawa Klabu yake Chelsea ilikataa moja kwa moja kuwa Mchezaji huyo hauzwi.
Leo Terry ametamka: ‘Mimi nipo Chelsea kwa moyo wangu wote, kwa siku zote! Kuhama? Haiwezekani!’
Pengine msimamo wa Terry ni habari murua kwa Chelsea ambayo imekuwa ikyumba kwa zaidi ya miaka miwili sasa huku ikibadilisha Mameneja mara 5 na kushinda Kombe moja tu na nalo ni la FA msimu uliopita.
Mido kuiaga Boro!!
Mchezaji wa Misri, Mido, ambae alitwangwa faini ya Mishahara ya wiki mbili baada ya kuchelewa kuripoti klabuni baada ya likizo, sasa atauzwa kwa Klabu nyingine ambayo imetoa ofa isiyoweza kukataliwa na Middlesbrough kufuatana na Meneja wao Gareth Southgate.
Southgate ametangaza kuwa Boro wameikubali ofa hiyo lakini ni juu ya Mido sasa kuikubali au la na pia kukubaliana na Klabu hiyo ambayo hakuitaja.
Msimu uliokwisha Mido alikuwa akichezea Wigan kwa mkopo na kwa sasa Middlesbrough imeshushwa Daraja kutoka Ligi Kuu na itacheza Coca Cola Championship msimu ujao.

No comments:

Powered By Blogger