Tuesday 28 July 2009

Uhamisho wapamba moto: Crouch katua Spurs, Ibrahimovic na Eto’o wabadilishana Klabu, Toure kuhama Arsenal kumfuata Adebayor?
Tottenham imemsaini Fowadi wa England Peter Crouch, miaka 28, kutoka Portsmouth kwa dau la Pauni Milioni 9.
Sasa anajumuika tena na Meneja Harry Redknapp ambae alikuwa Portsmouth kabla ya kuhamia Tottenham.
Nae Mchezaji wa Kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic amesaini mkataba wa miaka mitano na Barcelona akitokea Inter Milan alipokaa miaka mitatu na ambapo Barca wamelipa dau la Euro Milioni 45 pamoja na kumtoa Samuel Eto’oo kuhamia Inter na pia kuruhusu Alexander Hleb kucheza Inter kwa mkopo ikiwa ni makubaliano kati ya Klabu hizo mbili.
Wakati huo huo, Manchester City wako karibu sana kumsaini Mlinzi wa Arsenal Kolo Toure, umri miaka 28, kwa dau la Pauni Milioni 15.
Toure aliichezea Arsenal jana usiku huko Hungary kwenye mechi ya kirafiki na habari hizi za uhamisho pia ziliguswa na Arsene Wenger alietamka: ‘Tuataangalia nini kitatokea katika masaa 24 yajayo. Bado hamna kitu kilichokamilika. Tunao Msentahafu 7 ingawa Kolo ni Mchezaji mzuri.’

No comments:

Powered By Blogger