Wednesday 29 July 2009

MAN U 2 BOCA 1
Manchester United wakicheza mjini Munich Uwanja uitwao Allianz Arena wamewafunga magwiji wa Marekani ya Kusini Boca Juniors ya Argentina mabao 2-1 na kuingia Fainali ya Kombe la Audi.
Man U wanasubiri mshindi kati ya Bayern Munich au AC Milan watakaocheza leo.
Alikuwa ni Anderson alieipatia Man U bao la kwanza, hilo likiwa bao lake la kwanza kabisa kuifungia Man U [ukitoa la penalti Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya Chelsea] na alilifunga dakika ya 22 kwa frikiki nzuri sana.
Nae Luis Antonio Valencia, akicheza mechi yake ya kwanza kwa Man U, alifunga bao la pili dakika ya 41 na hilo likiwa pia bao lake la kwanza kwa Man U.
VIKOSI VILIKUWA:
Boca Juniors: Abbondanzieri; Soto, Lopez, Forlin; Diaz (Chavez 46), Battaglia, Riquelme (Marino 88), Insua (Gaitan 67), Lopez; Noir (Mouche 46), Palermo (Viatri 81).Akiba hawakucheza: Garcia (GK), Gunino, Krupoviesa, Philippe, Monzon.

Manchester United: Kuszczak; O'Shea, Cathcart, Brown (Ferdinand 37), Fabio (Evra 77); Valencia (Nani 68), Anderson (Fletcher 77), Carrick (Scholes 77), Park (Giggs 68); Rooney, Macheda (Berbatov 68).Akiba hawakucheza: Foster, Tosic, Vidic, Evans, Gibson.

No comments:

Powered By Blogger