Sunday 26 July 2009

Celtic wabeba Kombe la Wembley!
Klabu ya Scotland, Celtic, leo imebeba Kombe la Wembley walipoifunga Tottenham bao 2-0 magoli yote yakipatikana kipindi cha kwanza na kufungwa na Chris Killen, dakika ya 9, na Georgios Samaras, dakika ya 40.
Katika mechi ya kwanza Celtic iliibamiza El Ahly ya Misri mabao 5-0.
Tottenham walitoka suluhu na Barcelona 1-1
Man City wadodondoshwa Bondeni!
Manchester City wamemaliza ziara yao huko Afrika Kusini kwa kufungwa mechi ya pili kati ya tatu walizocheza na jana walipigwa bao 1-0 na Kaizer Chiefs kwa bao la utata baada ya mfungaji wa Kaizer Chiefs Jeffrey Ntuka kuumiliki mpira kwa mkono na kisha kufunga katika dakika ya 42.

Emmanuel Adebayor jana alicheza mechi yake ya kwanza akivaa Jezi ya Bluu ya Man City na akaikosesha bao la wazi dakika ya 55 alipofumua shuti juu ya posti.

No comments:

Powered By Blogger