Saturday 1 August 2009

Spurs yatwaa Kombe la Asia: Spurs 3 Hull 0
Tottenham Hotspurs, wakicheza Beijing, wameifunga Hull City mabao 3-0 na kushinda Kombe la Asia.
Mabao ya Spurs yalifungwa na Robby Keane, mawili, na Aaron Lennon bao moja.
Sir Bobby Robson afariki!
Meneja wa zamani wa England, Newcastle na Ipswich Town, Sir Bobby Robson, miaka 76, amefariki dunia.
Robson, aliewahi pia kuwa Kocha wa Klabu za PSV Eindhoven, Sporting Lisbon, Porto na Barcelona, amekuwa akisumbuliwa na kansa.
Mwaka 1990 aliifikisha England Nusu Fainali ya kombe la Dunia huko Italia lakini ikakosa kuingia Fainali baada ya kubwagwa kwa penalti na Ujerumani.
Roy Keane aipeleka Ipswich Town Kambi ya Jeshi kupata mafunzo ya kijeshi kuongeza nguvu!
Roy Keane, ambae sasa ni Meneja wa Ipswich Town Timu ambayo ipo Daraja la chini tu ya Ligi Kuu England na ambae ndio kwanza tu anaanza kazi hiyo na timu hiyo, ameipeleka Timu yake hiyo mpya kwenye Kambi ya Kijeshi ya Jeshi la Uingereza kupata mafunzo ya kijeshi ili kujenga stamina na kuongeza nguvu zaidi.
FK Vetra 0-3 Fulham
Wakicheza mechi yao ya kwanza ugenini kwenye Kombe jipya la EUROPA LEAGUE, Fulham wameishinda FK Vetra bao 3-0 huko Lithuania.

Timu hizi ztarudiana mjini London wiki ijayo Uwanja wa Craven Cottage nyumbani kwa Fulham.
Timu nyingine za Ligi Kuu zinazocheza EUROPA LEAGUE ni Aston Villa na Everton ambazo zitaanza kushirikishwa raundi ijayo kwani zilimaliza Ligi nafasi ya 5 na ya 6.

Fulham ilimaliza nafasi ya 7.

No comments:

Powered By Blogger