Wednesday 29 July 2009

UZI MPYA WA MAN U MECHI ZA UGENINI WAANIKWA!!
Mabingwa Manchester United wameuonyesha uzi wao mpya watakaoutumia kucheza mechi za ugenini za msimu wa 2009/10.
Jezi hizo ni za rangi nyeusi zikiwa na mstari wa v kifuani, bukta na stokingi pia ni nyeusi.
Man U watazivaa Jezi hizo kwa mara ya kwanza kesho huko Ujerumani watakapocheza na Bayern Munich au AC Milan kwenye Kombe la Audi.
Mechi hiyo ya kesho itakuwa ni ama Fainali ya Kombe hilo au mechi ya kutafuta mshindi wa tatu yote yakitegemea matokeo ya mechi za leo wakati ni Man U v Boca Juniors na Bayern Munich v AC Milan.

No comments:

Powered By Blogger