Thursday 30 July 2009

FIFA: VUVUZELA RUKSA FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010 HUKO BONDENI!!!!
FIFA imethibitisha kuwa Vuvuzela, zile tarumbeta za plastki za kila rangi ambazo Mashabiki wa Afrika Kusini ni utamaduni wao kuingia nazo uwanjani na kuzipuliza zikitoa sauti mithili ya Kundi la Tembo linalofanya uvamizi, zitaruhusiwa kwenye mechi za Fainali za Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini.
Vuvuzela lilipata umaarufu maradufu hivi karibuni wakati wa Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara la huko Afrika Kusi lililobebwa na Brazil huku baadhi ya Timu, hasa Spain, kudai linaudhi na ndilo lililowafanya wakose kushinda.
FIFA wamesema Vuvuzela ni ruksa labda ibainike ni hatari kwa usalama wa watu.

No comments:

Powered By Blogger