Saturday, 1 August 2009

Torres: “England ni bora!”
Straika wa Liverpool kutoka Spain, Fernando Torres, amesisitiza kuwa katika uliwengu wa soka England ni bora na Ligi Kuu ndio ligi bora duniani.
Alipoambiwa kuwa kufuatia jinsi vigogo wa Spain, Real Madrid na Barcelona, walivyopapia kununua Wachezaji inaelekea sasa La Liga ndio itatawala, Torres alibisha na kusisitiza bado England ni bora.
Torres alitamka: “Soka ya England ina wafuasi wengi sana dunia nzima! Na hilo si kwa ajili ya Wachezaji tu bali ni kwa sababu ya historia, utamaduni, uwazi na uaminifu, na pia jinsi Viwanja vinavyofurika watu!”
Robinho alimbembeleza Hughes Elano asiuzwe!
Robinho ametoboa kuwa alikwenda kumsihi Meneja wake wa Manchester City, Mark Hughes, asimuuze Mchezaji mwenzake kutoka Brazil, Elano.
Man City imemuuza Elano kwa Klabu ya Uturuki Galataaray kwa Pauni Milioni 8.
Robinho alisema kwa majonzi: “Imenisikitisha sana! Alikuwa mwenzangu na rafiki mkubwa! Namuombea mema kwa Klabu yake mpya.”

No comments:

Powered By Blogger