Wednesday, 29 July 2009

Kombe la AUDI Ujerumani: Makocha wa Klabu zinazoshiriki waikandya Real Madrid!
Kombe la Audi ili kusherehekea miaka 100 ya Kampuni ya kutengeneza magari aina ya Audi linaanza kushindaniwa leo huko Ujerumani na washiriki ni Klabu za Boca Juniors kutoka Argentina, Klabu za Ulaya wenyeji Bayern Munich, AC Milan na Manchester United.

Jana kwenye mahojiano ya pamoja na Waandishi wa Habari, Makocha wa Timu 3 Wakongwe wa Ulaya wote kwa pamoja waliishambulia Real Madrid kwa msimamo wao wa kununua Wachezaji kwa bei mbaya na wote walionyesha kushangazwa na kutojua jinsi Timu itakavyopangwa kwani mpaka sasa Timu hiyo haina Walinzi wazuri na hivyo itakosa uwiano kiwanjani.
Makocha wa Manchester United na AC Milan, Sir Alex Ferguson na Leonardo, wote wamewapoteza Wachezaji wao nyota, Ronaldo na Kaka, waliokimbilia Real kwa kitita cha kustusha. Kocha wa Bayern Munich, Louis van Gaal, mpaka sasa anapigana nyota wake Franck Ribery asikimbilie Real Madrid.
Ferguson alisema Real Madrid itakuwa haina uwiano Uwanjani na hata alimtahadharisha Ronaldo kuwa itakuwa si ajabu kama akiishia kucheza Sentahafu Klabuni hapo! Ferguson aliongeza tofauti na Real, Barcelona wamekuwa wakijenga Timu polepole kwa kununua Mchezaji mmoja au wawili kila msimu.
Ferguson alitamka: ‘Kuna mfano mzuri huko England katika miaka ya nyuma Sunderland ilitumia pesa nyingi kununua Wachezaji na ikabatizwa jina Benki ya England! Hawakufanikiwa na matokeo yake wakashushwa Daraja! Sisemi Real watashuka ila watapata matatizo upangaji Timu!’
Mameneja wenzake wakamuunga mkono Ferguson na Van Gaal akasema kuwa kuna Makocha, kama Ferguson na yeye, wanaweza kuunda Timu upya lakini hadhani Real itakuwa tishio kwa sababu timu inajengwa na si kununuliwa!
Nae Leonardo, ingawa alikubali Real wana uzito kifedha, aliwakumbusha watu kuwa wakati Real ilipokuwa na ‘Galactico’ [vizito] Zidane, Figo na Beckham timu ilipoteza mwelekeo kadiri ‘vizito’ wengine walipoongezwa na akasisitiza ni vigumu kuwamiliki Masupastaa wote kama Kaka, Ronaldo na Benzema katika timu moja.
MATOKEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE: RAUNDI ZA MCHUJO
Jumanne, 28 Julai 2009
Anderlecht 5 v Sivasspor 0
FC Aktobe 0 v Maccabi Haifa 0
FK Baku 0 v Levski Sofia 0
Sparta Prague 3 v Panathinaikos 1
RATIBA LEO:
-KOMBE LA ASIA:
West Ham v Tottenham
Hull City v Beijing Guoan
-MECHI YA KIRAFIKI:
Hannoverscher v Arsenal

No comments:

Powered By Blogger