Saturday 1 August 2009

Mido arudi kwao Misri!!
Mido amehama Klabu yake Middlesbrough iliyoshuhwa Daraja kutoka Ligi Kuu England na kurudia kwao kwenye Klabu ya Zamalek alikoanzia kucheza soka.
Zamalek imeilipa Boro Pauni Milioni 4 ili Mido acheze huko kwa mkopo kwa msimu mmoja na itawabidi waongeza Pauni Milioni 1 zaidi ikiwa watataka kumchukua moja kwa moja.
Baada ya Boro kushushwa Daraja, Mido, umri miaka 26, aligoma kurudi kuichezea Timu hiyo.
Mido huko nyuma amewahi kuzichezea Klabu za Gent, Ajax, Celta Vigo, Marseille, na Wigan katika kipindi cha miaka 9 iliyopita.
Mido alitimuliwa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Misri baada ya kuzozana na Kocha wa Misri Hassan Shehata alipoamuliwa kutoka uwanjani ili aingizwe Mchezaji mwingine katika mechi ya Nusu Fainali ya kugombea Kombe la Mtaifa ya Afrika mwaka 2006 dhidi ya Senegal.

No comments:

Powered By Blogger