Tuesday 28 July 2009

AUDI CUP KESHO HUKO UJERUMANI: Man U v Boca Juniors na Bayern Munich v AC Milan
Kesho huko Ujerumani saa moja na nusu usiku saa za bongo, Manchester United wanashuka dimbani kupambana na vigogo wa Marekani ya Kusini, Boca Juniors kutoka Argentina, kwenye pambano la kwanza kugombea Kombe la Audi na mechi hiyo itafuatiwa na ile ya Wenyeji Bayern Munich kucheza na AC Milan ya Italy.
Washindi wa mechi hizo watakutana Fainali Alhamisi saa 3 dakika 45 usiku mechi itakayotanguliwa na ile ya kutafuta Mshindi wa Tatu ambayo itachezwa baina ya timu zitakazofungwa kesho.

No comments:

Powered By Blogger