Sunday 30 May 2010

England 2 Japan 1, Goli zote wafunga Japan!!!
Magoli mawili ya kujifunga wenyewe leo yamewapa ushindi England wa bao 2-1 dhidi ya Japan huko Graz, Austria katika mechi ambayo Kocha wa England aliwaacha benchi Mastaa kadhaa na kimchezo England walipwaya mno.
Japan walipata bao lao dakika ya 6 baada ya Beki Marcus Tulio Tanaka kuwasha bunduki baada ya kona ya Yasuhito Endo na mpira kumpita Kipa David James.
Hadi mapumziko Japan walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili, dakika ya 56, Frank Lampard alishindwa kufunga penalti iliyookolewa na Kipa Eiji Kawashima.
England walipewa penalti hiyo Endo alipounawa mpira kufuatia frikiki ya Lampard.
Kipindi hicho cha Pili, Capello aliwatoa Wachezaji watano kina David James, Johnson, Huddlestone, Walcott na Bent na kuwaingiza Joe Hart, Jamie Carragher, Joe Cole, Shaun Wright-Phillips na Steven Gerrard.
Mabadiliko hayo yalileta uhai kwa England na presha yao ilizawadiwa kwa Japan kujifunga wenyewe bao mbili.
Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 72 kufuatia krosi ya Joe Cole kupigwa kichwa na beki wa Japan Marcus Tulio Tanaka na kutinga wavuni.
Bao la pili pia lilitokana na krosi, na safari hii ilikuwa krosi ya Ashley Cole, iliyofungwa na Beki wa Japan Nakazawa.
Vikosi vilikuwa:
England: David James (Joe Hart, 46), Glen Johnson (Jamie Carragher, 46), Ashley Cole, Tom Huddlestone (Steven Gerrard, 46), Rio Ferdinand, John Terry, Theo Walcott (Shaun Wright-Phillips, 46), Frank Lampard, Darren Bent (Joe Cole, 46), Wayne Rooney, Aaron Lennon (Emile Heskey, 77).
Japan: Eiji Kawashima, Yuji Nakazawa, Marcus Tanaka, Yuto Nagatomo, Yusuyuki Konno, Yasuhito Endo (Keiji Tamada, 86), Makoto Hasebe, Abe Yujki, Keisuke Honda, Yoshito Okubu (Daisuke Matsui, 72), Shinji Okazaki (Takayuki Morimoto, 65).

No comments:

Powered By Blogger