Thursday, 3 June 2010

Benitez mguu nje Anfield
Meneja wa Liverpool Rafael Benitez yupo njiani kuondoka hapo Anfield baada ya uongozi wa Klabu kumpa ofa ya Pauni Milioni 3 ili aende zake.
Benitez alisaini Mkataba wa Miaka mitano Mwaka 2009 lakini hamna mafanikio yeyote yaliyopatikana huku Klabu ikiwa inaandamwa na Madeni ya zaidi ya Pauni Milioni 350.
Wamiliki wa Liverpool, Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gillet, wamekuwa wakitafuta mnunuzi bila mafanikio.
Habari toka ndani ya Klabu hiyo zimesema upo uhakika Benitez ataondoka Klabuni hapo wikiendi hii huku Inter Milan ikitajwa kuwa ndiko aendako kuchukua nafasi ya Jose Mourinho aliehamia Real Madrid.
Liverpool inasemekana inataka kumuondoa Benitez kwa kumpa ofa hiyo ili kukwepa kumlipa Pauni Milioni 16 ikitaka kumtimua kabla ya Mkataba wake kumalizika.
Grant athibitishwa Meneja West Ham
Avram Grant amethibitishwa kama Meneja mpya wa West Ham na amepewa Mkataba wa Miaka Minne.
Grant anachukua nafasi ya Gianfranco Zola alietimuliwa.
Grant amekaririwa akisema anasikia fahari kwa kuteuliwa Meneja wa West Ham.
Wachezaji England wapewa namba zao za Jezi
Kocha wa England, Fabio Capello, ametangaza namba za Jezi za Wachezaji wake 23 wa Fainali za Kombe la Dunia huku Joe Cole, David James na Peter Crouch wakiwa ndani ya Listi ya Wachezaji 11 wa kwanza.
Kipa David James amepewa Jezi namba 1, Crouch namba 9 na Joe Cole namba 11.
Ingawa nambari za Jezi si kigezo cha kuwa Wachezaji hao ndio wapo Timu ya Kwanza, lakini Wataalam wanahisi hicho ni kipimo tosha cha kuonyesha Wachezaji gani wapo mbele katika uteuzi.
Nahodha wa England, Rio Ferdinand, ametamka: “Hakuna Mchezaji alie salama. Meneja huyu haogopi kuwabwaga Wachezaji wenye sifa akiwaona hawachezi vizuri. Yeye anashughulikia kila kitu vizuri tu.”
England watacheza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia Juni 12 dhidi ya USA Uwanja wa Royal Bafokeng Mjini Rustenburg.
Timu hiyo ilitua Johannesburg leo asubuhi ikitokea London na ilienda moja kwa moja Kambini kwao Kituo cha Michezo cha Royal Bafokeng kilichopo Rustenburg.
Kikosi kamili cha England na Namba za Jezi:
1. David James
2. Glen Johnson
3. Ashley Cole
4. Steven Gerrard
5. Rio Ferdinand
6. John Terry
7. Aaron Lennon
8. Frank Lampard
9. Peter Crouch
10. Wayne Rooney
11. Joe Cole
12. Robert Green
13. Stephen Warnock
14. Gareth Barry
15. Matthew Upson
16. James Milner
17. Shaun Wright-Phillips
18. Jamie Carragher
19. Jermain Defoe
20. Ledley King
21. Emile Heskey
22. Michael Carrick
23. Joe Hart

No comments:

Powered By Blogger