Tuesday 1 June 2010

Wolves wamsaini Van Damme
Pengine Wadau watashtuka kuona Wolves imemsaini Van Damme lakini huyu si Yule Mcheza Sinema bali ni Beki wa Ubelgiki anaechezea Klabu ya Anderlecht aitwae Jelle Van Damme, miaka 26, na amesaini Mkataba wa Miaka mitatu kwa dau ambalo halikutangazwa.
Mwaka 2004/5, Van Damme alikuwa na Southampton na aliwahi kucheza mechi za Ligi Kuu.
Pia ameshawahi kuichezea Werder Bremen na ameichezea Timu ya Taifa ya Ubelgiji mechi 26.
Mtu 23 za Ivory Coast zatajwa!
Kocha wa Ivory Coast, Sven-Goran Eriksson, ametangaza majina ya Wachezaji 23 yatakayowasilishwa FIFA hapo kesho kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia na Wachezaji maarufu waliobwagwa ni Bakary Kone na Kanga Akale.
Yale Majina mengine mazito ya kina Didier Drogba, Salamon Kalou, Aruna Dindane na Seydou Doumbia yapo kama ilivyotegemewa.
Ivory Coast wapo Kundi G pamoja na Brazil, Ureno na Korea Kaskazini.
Kikosi kamili:
MAKIPA: Boubacar Barry (Lokeren, Belgium), Aristides Zogbo (Maccabi Netanya, Israel), Daniel Yeboah (Asec, Ivory Coast).
MABEKI: Souleymane Bamba (Hibernian, Scotland), Arthur Boka (VB Stuttgart, Germany), Benjamin Brou Angoua (Valenciennes, France), Guy Demel (Hamburg SV, Germany), Emmanuel Eboue (Arsenal, England), Steve Gohouri (Wigan Athletic, England), Siaka Tiene (Valenciennes, France), Kolo Toure (Manchester City, England).
VIUNGO: Jean-Jacques Gosso Gosso(Monaco, France), Abdelkader Keita (Galatasaray, Turkey), Emmanuel Kone (International Curtea Arges, Romania), Gervinho (Lille, France), Koffi N'Dri Romaric (Sevilla, Spain), Cheik Ismael Tiote (Twente Enschede, Holland), Yaya Toure (Barcelona, Spain), Didier Zokora (Sevilla, Spain).
MAFOWADI: Aruna Dindane (Lekhwiya, Qatar), Didier Drogba (Chelsea, England), Salomon Kalou (Chelsea, England), Bakary Kone (Olympique Marseille, France).
McCarthy nje Afrika Kusini
Carlos Alberto Parreira hakumchukua Straika wa West Ham Benni McCarthy katika Timu yake ya Wachezaji 23 ya Afrika Kusini ambao ndio Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia litaloanza Juni 11.
Lakini Wachezaji wengine walio Ligi Kuu England, kama vile Steven Pienaar wa Everton na Mchezaji wa Fulham Kagiso Dikgacoi wamo.
Kikosi hicho kitaongozwa na Aaron Mokoena ambae ni Mlinzi wa Portsmouth.
McCarthy ndie Mchezaji anaeongoza kwa kufunga goli nyingi kwa Afrika Kusini na ana goli 31 katika mechi 79 alizochezea Timu ya Taifa na alikuwemo kwenye Vikosi vya Bafana Bafana vya Kombe la Dunia Mwaka 1998 na 2002.
Lakini tangu ajiunge na West Ham Februari 1 kutokea Blackburn Rovers amekuwa na maumivu ya goti na wengi wamekuwa wakimlaumu kwa kuongezeka uzito.
Afrika Kusini wapo Kundi A pamoja na Mexico, Uruguay na Ufaransa.
Kikosi kamili:
MAKIPA: Moeneeb Josephs (Orlando Pirates), Itumeleng Khune (Kaizer Chiefs), Shu-Aib Walters (Maritzburg United)
MABEKI: Matthew Booth, Siboniso Gaxa (both Mamelodi Sundowns), Bongani Khumalo (SuperSport United), Tsepo Masilela (Maccabi Haifa), Aaron Mokoena (Portsmouth), Anele Ngcongoa (Racing Genk), Siyabonga Sangweni (Lamontville Golden Arrows), Lucas Thwala (Orlando Pirates).
VIUNGO: Lance Davids (Ajax Cape Town), Kagisho Dikgacoi (Fulham), Thanduyise Khuboni (Lamontville Golden Arrows), Reneilwe Letsholonyane (Kaizer Chiefs), Teko Modise (Orlando Pirates), Surprise Moriri (Mamelodi Sundowns), Steven Pienaar (Everton), MacBeth Sibaya (Rubin Kazan), Siphiwe Tshabalala (Kaizer Chiefs).
MAFOWADI: Katlego Mphela (Mamelodi Sundowns), Siyabonga Nomvete (Moroka Swallows), Bernard Parker (FC Twente).

No comments:

Powered By Blogger