Kisu kumuokoa Drogba acheze Bondeni
Ushiriki wa Nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba Fainali za Kombe la Dunia huenda ukaokolewa kwa kufanyiwa operesheni ili kuunga mfupa uliovunjika kwenye kiwiko cha mkono wake wa kulia na baada ya upasuaji huo atahitaji siku 10 kupona.
Drogba aliumizwa jana alipovaana na Sentahafu wa Japan, Marcus Tulio Tanaka, mzaliwa wa Brazil, katika mechi ya kirafiki huko Uswisi ambayo Ivory Coast walishinda 2-0.
Kocha wa Ivory Coast, Sven-Goran Eriksson, amesema bado ipo nafasi kwa Drogba kucheza Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza huko Africa Kusini Juni 11 na mechi ya kwanza kwa Ivory Coast ni Juni 15 dhidi ya Ureno.
Ivory Coast wapo Kundi G pamoja na Brazil, Ureno na Korea Kaskazini.
Eriksson alisema: “Huenda akafanyiwa operesheni na huenda akacheza Fainali. Amevunjika mfupa karibu na kiwiko lakini atamwona Speshelisti. Tutajua kesho!”
Drogba ndie Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England kwa Msimu ulioisha hivi karibuni wa Mwaka 2009/10.
RATIBA MECHI ZA KIRAFIKI ZA KIMATAIFA
Jumamosi, Juni 5
Holland v Hungary
South Africa v Denmark
Australia v USA
Ghana v Latvia
Slovakia v Costa Rica
Algeria v UAE
Romania v Honduras
Serbia v Cameroon
Switzerland v Italy
No comments:
Post a Comment