Friday 4 June 2010

Liverpool waanza msako wa Meneja mpya
Baada ya kupeana mkono wa kwaheri kufuatia makubaliano ya pamoja na Rafael Benitez, Liverpool inaanza msako wa kumpata Meneja mpya na jukumu hilo limetundikwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Christian Purslow, na Kenny Daglish, ambae aliwahi kuwa Meneja wa Liverpool hapo zamani na sasa ni Balozi wa Chuo cha Soka Klabuni humo.
Majina ya Warithi yanayotajwa ni Roy Hodgson wa Fulham, Martin O’Neill wa Aston Villa na Mark Hughes, Meneja wa zamani wa Manchester City.
Lakini baadhi ya Wachezaji wa zamani wa Liverpool, wakiwemo Kipa kutoka Zimbabwe, Bruce Grobbelaar, na Jamie Redknapp, wanataka Kenny Daglish ashike hatamu.
Baba aacha kazi ende Bondeni kumwona Mwanawe Chicharito!!
Baba Mzazi wa Mchezaji mpya wa Manchester United, Javier ‘Chicharito’ Hernandez, anaechezea Timu ya Mexico ambayo imo kwenye Fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Afrika Kusini Juni 11, ameamua kuacha kazi yake ili asafiri kwenda Afrika Kusini kumshuhudia Mwanawe akicheza Fainali hizo.
Baba huyo, Hernandez, ni Meneja wa Timu ya Rezevu ya Klabu ya Chivas ya huko Mexico, ambao ni vigogo huko, aliomba ruhusa lakini akanyimwa na ndipo alipoamua kuacha kazi.
Baba huyo wa Chicharito amesema: “Niliomba ruhusa nikatizame Kombe la Dunia wakakataa. Nikakaa chini na Familia yangu na tukaamua niache kazi ili niende Afrika Kusini kumwona Mwanangu akicheza. Kwa hilo, kazi si muhimu. Ni uamuzi mzito lakini lazima ujue hapa Duniani hatuishi milele. Waajiri wapo milele, lakini mtu huko milele.”

No comments:

Powered By Blogger