Saturday 5 June 2010

Mastaa wazidi kupukutika Kombe la Dunia!!
Walianza Ballack, Essien, Rio na sasa Mikel huku Drogba…………….!
Kiungo wa Nigeria, John Mikel Obi, hatacheza Kombe la Dunia baada ya kuthibitika goti lake alilokuwa akiliuguza halitapona mapema.
Mikel anaungana na Mastaa wengine wa Klabu yake Chelsea, kina Ballack, Michael Essien na huenda pia Drogba, kuwa nje ya Kombe la Dunia baada ya kuumia.
Mikel alifanyiwa operesheni ndogo ya goti Mwezi Mei na inasemekana hajapona vizuri.
Msemaji wa Timu ya Nigeria amesema imebidi wamwache baada ya mwenyewe Mikel kujiona hajapona vizuri na kuendelea kuwepo na Nigeria kungesababisha kupata athari zaidi.
Nafasi ya Mikel imechukuliwa na Brown Ideye ambae ni Straika kutoka Klabu ya Ufaransa Sochaux na Ideye hajawahi kuichezea Nigeria hata mara moja.
Nigeria wapo Kundi B pamoja na Argentina, Ugiriki na Korea Kusini na watacheza mechi yao ya kwanza Juni 12 dhidi ya Argentina.

No comments:

Powered By Blogger