Rio nje Kombe la Dunia
Nahodha wa England, Rio Ferdinand, hatacheza Kombe la Dunia baada ya kuumizwa goti lake la mguu wa kushoto leo mazoezini huko Rustenburg, Afrika Kusini.
Inasemekana Rio aliumizwa goti hilo baada ya kuvaana na Emile Heskey kwenye mazoezi.
England imemwita Beki wa Tottenham, Michael Dawson, kuchukua nafasi ya Rio Ferdinand.
Dawson alikuwemo kwenye Kikosi cha awali cha Wachezaji 30 lakini aliachwa Siku ya Jumanne baada ya Kikosi hicho kupunguzwa na kuwa Wachezaji 23 wa mwisho.
Sasa Unahodha atachukua Steven Gerrard ambae alikuwa Naibu wa Rio.
Kombe la Dunia kwa Drogba ni hatihati!!
Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba, huenda akalikosa Kombe la Dunia kufuatia kuvunjika kwa kiwiko chake cha mkono wa kulia.
Drogba aliumizwa kwenye mechi ya kirafiki leo huko Switzerland walipocheza na Japan ambayo Ivory Coast walishinda 2-0 alipogongana na Beki wa Japan Marcus Tulio Tanaka.
Ingawa kulikosa Kombe la Dunia hakujathibitishwa na Viongozi wa Ivory Coast lakini Beki wa Timu hiyo anaichezea Manchester City, Kolo Toure, amedai Drogba hawezi kucheza Fainali hizo na ameambiwa hilo na mwenyewe Drogba.
Hata hivyo mpaka sasa habari hizo hazijathibitishwa.
No comments:
Post a Comment