Monday 31 May 2010

Mourinho atua Real na kutamba: “Mimi ni Jose Mourinho na sibadiliki! Nimetua na vipaji vyangu na kasoro zangu!”
Leo Jose Mourinho ametangazwa rasmi kama Meneja mpya wa Real Madrid kuchuku nafasi ya Manuel Pellegrini kutoka Chile na amesaini Mkataba wa Miaka minne.
Mourinho, mwenye Miaka 47, anakuwa Meneja wa 11 wa Real katika kipindi cha Miaka 7 iliyopita.
Real Madrid haijatwaa Kombe lolote kwa Miaka miwili sasa na uteuzi wa Mourinho ambae wiki moja iliyopita alitwaa Kombe la Klabu Bingwa akiwa na Inter Milan ni hatua ya kurekebisha kasoro hiyo kwa Timu iliyotumia zaidi ya Pauni Milioni 200 kuwanunua Masupastaa Ronaldo, Kaka, Alonso na Benzema hapo Mwaka jana.
HISTORIA YA MOURINHO KAMA MENEJA
-Benfica (2000)
-Uniao de Leiria (2000-02)
-Porto (2002-04) –Ubingwa wa Ligi mara 2, Kombe la Ureno, UEFA Cup mara 1, UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara 1.
-Chelsea (2004-07) –Ubingwa wa Ligi Kuu mara 2, Carling Cup mara 2, FA Cup mara 1.
-Inter Milan (2008-10) -Ubingwa Serie A mara 2, Coppa Italia mara 1, UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara 1.
Everton yamsaini Beckford
Everton imemsaji Straika hatari Jermaine Beckford kwa Mkataba wa Miaka minne na Mchezaji huyo kutoka Leeds United amesajiliwa kama Mchezaji huru kwa vile Mkataba wake na Leeds umemalizika.
Beckford ndie alieiwezesha Leeds kupanda Daraja na Msimu ujao itacheza Daraja la Coca Cola Championship ambalo liko chini tu ya Ligi Kuu.
Mchezaji huyo mwenye miaka 26 aliifungia Leeds mabao 31 Msimu uliopita na moja ya hayo ni lile bao lililowang’oa Manchester United kwa bao 1-0 kwenye Raundi ya 3 ya FA Cup Uwanjani Old Trafford Mwezi Januari.

No comments:

Powered By Blogger