Friday 4 June 2010

Janja ya Korea Kaskazini, FIFA Gundua!!!!!
Korea Kaskazini walitua Afrika Kusini wakiwa na Straika mmoja akitajwa kama Kipa wao wa tatu kama FIFA inavyotaka kwamba Listi ya Wachezaji 32 kwa Nchi zote zilizo Fainali ya Kombe la Dunia ziwe na Makipa watatu lakini mpango huo umepigwa chini na FIFA.
FIFA imewaambia Korea Kaskazini kuwa Mchezaji Kim Myong-won, ambae kawaida ni Straika, ataruhusiwa kucheza kama Kipa tu kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa vile jina lake limesilishwa kwao kuwa ni Kipa katika Listi ya mwisho ya Wachezaji 32 ambazo Nchi zote zilizoko Fainali Kombe la Dunia zilitakiwa kuwasilisha Juni 1.
Kocha wa Korea Kaskazini, Kim Jong-hun, alitangaza Majina ya Makipa wawili tu na kumtaja Straika Kim kuwa ni Kipa wa Tatu.
Korea Kaskazini wako Kundi G pamoja na Brazil, Ivory Coast na Ureno.
FIFA imetoa stetimenti kuelezea hali hiyo ya Korea Kaskazini na imesema: “Listi za Wachezaji 32 kwa kila Timu zilizowasilishwa kwetu Juni 1 ni za mwisho na haziwezi kubadilishwa. Listi hiyo ya Wachezaji 32 inataka Makipa wawe watatu. Kitu pekee kinachoweza kubadili listi hizo ni endapo Mchezaji ataumia vibaya Masaa 24 kabla ya Mechi ya kwanza, Mchezaji huyo anaweza kubadilishwa. Wachezaji watatu waliotajwa kama Makipa wanaruhusiwa kucheza nafasi ya Kipa tu kwenye Fainali hizi za Kombe la Dunia na hili limetangazwa kwa kila Timu. Hivyo Kim Myong-won haruhusiwi kucheza kama Straika.”

No comments:

Powered By Blogger