Tuesday 16 September 2008


CHELSEA WASHINDA RUFAA YA JOHN TERRY!!!

Klabu ya Chelsea imeshinda rufaa waliyokata kwa FA kupinga kadi nyekundu aliyopewa Nahodha wao John Terry kwenye mechi na Manchester City iliyochezwa Uwanja wa City of Manchester ambayo Chelsea walishinda 3-1 wikiendi iliyokwisha.
Hivyo, Terry yuko huru kuikabili Man U watakapocheza Jumapili kwenye mechi ya LIGI KUU uwanjani Stamford Bridge.

MICHAEL CARRICK NJE WIKI SITA!!!

Kiungo wa Mabingwa Man U Michael Carrick atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 6 baada ya kuthibitishwa amevunjika mfupa mguuni baada ya kuumizwa na Yossi Benayoun Jumamosi katika mechi ya Liverpool na Man U.
Huu ni mkosi kwa Carrick kwani alikuwa ndio kwanza tu amerudi uwanjani baada ya kuwa nje kwa wiki 3 baada ya kuumia enka.

No comments:

Powered By Blogger