Thursday 18 September 2008

MAPYA:

-ESSIEN AFANYIWA UPASUAJI

Kiungo wa Chelsea Michael Essien leo amepasuliwa goti lake huko Ufaransa baada ya kuumizwa wakati akichezea nchi yake Ghana ilipocheza na Libya mjini Tripoli wiki iliyokwisha kwenye mechi ya kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini mwaka 2010.
Inakadiriwa Essien atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 6.

-RAY WILKINS ATEULIWA MENEJA MSAIDI CHELSEA

Ray Wilkins aliewahi kuzichezea klabu za Chelsea, Man U, AC Milan, PSG na QPR ameteuliwa kuwa msaidi wa Meneja Luis Felipe Scolari kuchukua nafasi ya Steve Clarke alieacha kazi juzi kwenda kujiunga na Meneja mpya wa West Ham Gianfranco Zola.
Ray Wilkins alishawahi kuwa na nafasi hiyo hapo Chelsea kati ya mwaka 1998 na 2000 wakati Meneja wa Chelsea alikuwa Gianluca Vialli.

-FA KUCHUNGUZA KAULI YA SIR ALEX FERGUSON KUHUSU KUTENGULIWA KADI YA JOHN TERRY

Chama cha Soka Uingereza kimetamka kinachunguza kauli za Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson alipomponda Bosi wa Marefa Keith Hackett kwa kuleta shinikizo ili Nahodha wa Chelsea John Terry afutiwe kadi nyekundu.
Meneja huyo wa Manchester United, Sir Alex Ferguson juzi alibwata: 'Hacket alimlazimisha Refa Mark Halsey aifute kadi nyekundu iwe njano lakini refa alipogoma sasa kashushwa na wikiendi hii hachezeshi mechi za LIGI KUU! Atachezesha mechi ya Daraja la Tatu [inaitwa LEAGUE TWO]! Angekuwa mchezaji wa Man U Hackett asingefanya hili!!!'
Wikiendi hii Refa Mark Halsey kapangiwa kuchezesha mechi ya LEAGUE TWO kati ya Chester na Shrewsbury.

No comments:

Powered By Blogger