Monday, 15 September 2008

LIGI KUU UINGEREZA:
STOKE CITY 2 EVERTON 3
Everton jana waliwafunga nyumbani kwao Stoke City timu iliyopanda daraja msimu huu mabao 3-2 katika mechi ya vuta ni kuvute.
Everton walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Mnigeria Yakubu dakika ya 41 na kwenye dakika ya 51 Victor Anichebe akafunga la pili kwa Everton.
Stoke City wakajitutumua na kufunga la kwanza kwa bao la Olofinjana dakika ya 55 na kisha mlinzi wa Everton Jagielka akajifunga mwenyewe na kufanya ngoma kuwa 2-2.
Lakini kwenye dakika ya 77 kona iliyopigwa na Arteta ilimaliziwa na Tim Cahill kwa kichwa safi na kuwapa ushindi Everton wa mabao 3-2.
Kwenye mechi hii Meneja wa Everton David Moyes alilambwa kadi nyekundu na Refa Alan Wiley baada ya kulalamika kwa nguvu kwa Refa wa akiba kuhusu timu yake kunyimwa penalti ya dhahiri na hivyo ikabidi aondolewa kwenye benchi la akiba na kwenda kumalizia mechi kwenye jukwaa la watizamaji.
LIGI KUU inaendelea leo usiku saa 4 [bongo time] kwa mechi kati ya Tottenhan na Aston Villa.

No comments:

Powered By Blogger