Wednesday 17 September 2008

LIVERPOOL NA CHELSEA WAANZA VYEMA

-AS ROMA WAPIGWA MWELEKA KWAO NA TIMU MPYA!
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ameiongoza vyema timu yake na kuifungia mabao mawili na kuwashinda Marseille kwa mabao 2-1 katika mechi ya KUNDI D.
Marseille wakiwa uwanjani kwao Stade Velodrome walitangulia kupata bao dakika ya 23 baada ya Nahodha wao Lorik Cana kuvunja mtego wa kuotea na kutikisa nyavu.
Dakika chache baadae Steven Gerrard akasawazisha kwa bao murua na akafunga la pili kwa penalti baada ya Torres kufanyiwa madhambi.
Katika mechi nyingine ya kundi hili la Liverpool KUNDI D, PSV iliadhiriwa kwa mabao 3-0 na Atletico Madrid.
Nao Chelsea wakichezea Uwanja wao Stamford Bridge waliwabandika Bordeaux ya Ufaransa mabao 4-0 katika mechi ya KUNDI A.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Frank Lampard, Joe Cole, Florent Malouda na Nicolas Anelka.
Katika mechi nyingine ya kundi hili la Chelsea timu iliyotegemewa sana AS Roma ikicheza nyumbani kwake ilipigwa mweleka na timu mpya na isiyojulikana kabisa kwenye michuano hii CFR Cluj kutoka Romania kwa mabao 2-1.
Christian Panucci aliwapa AS Roma bao la kutangulia dakika ya 17 lakini Juan Culio kutoka Argentina aliisawazishia timu yake CFR Cluj kwenye dakika ya 27 na tena kupachika bao la ushindi dakika ya 49.

MATOKEO KAMILI NI:

KUNDI A:
Chelsea 4-0 Bordeaux;
Roma 1-2 CFR Cluj-Napoca;

KUNDI B:
Panathinaikos 0-2 Inter Milan ;
Werder Bremen 0-0 Anorthosis Famagusta;

KUNDI C:
Barcelona 3-1 Sporting;
Basle 1-2 Shakhtar Donetsk;

KUNDI D:
Marseille 1-2 Liverpool;
PSV 0-3 Atletico Madrid;

No comments:

Powered By Blogger