Friday 19 September 2008

MECHI YA VIGOGO KESHO: vimbwanga vyaanza!!

-FERGUSON: CHELSEA WANATUOGOPA!!

-SCOLARI ACHOCHEA: RONALDO ANAKARIBISHWA CHELSEA!!

-WENGER: BORA DRO KWANI KILA TIMU ITAPOTEZA POINTI!!

Meneja Sir Alex Ferguson wa Manchester United amesisitiza kuwa Chelsea wanajua wazi kikosi chake kina uwezo wa kushinda nyumbani kwa Chelsea Uwanja wa Stamford Bridge.
Mpaka sasa Chelsea hawajafungwa katika mechi 84 za ligi walizochezea uwanja wao wa Stamford Bridge na mara ya mwisho kufungwa hapo ilikuwa mwaka 2005.
Mpaka sasa Chelsea imecheza mechi 4 na ina pointi 10 wakati Man U ina pointi 4 kwa mechi 3.
Endapo Chelsea watashinda basi timu ya Luiz Felipe Scolari watakuwa mbele kwa pointi tisa zaidi ya Man U kitu ambacho Sir Alex Ferguson hataki kitokee ingawa timu yake imecheza mechi moja pungufu
Ferguson alisema: "Chelsea wanajua fika Manchester United wanaweza kushinda Jumapili. Wao ni timu nzuri na wameaanza ligi vizuri. Lakini timu yangu ina uwezo. Tuna kazi kubwa lakini wachezaji wangu wana ari kubwa.”
Ferguson akaongeza: “Ronaldo ananikera kila dakika anataka kuanza Jumapili. Amefanya mazoezi mazito na yuko fiti.”
Nae Luiz Felipe Scolari ametia utambi mechi hii kwa kudai atapendelea sana kama Cristiano Ronaldo atakuja kuwa mchezaji wa Chelsea kwani anaamini ni Mchezaji Bora Duniani jambo ambalo bila shaka limelengwa kumuudhi Sir Alex Ferguson.
Scolari aliwahi kumfundisha Ronaldo wakati akiwa Meneja wa Timu ya Taifa ya Ureno ambayo Ronaldo huchezea.
Nae Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, amesema wao wanaomba timu zote zipoteze pointi kwa kutoka suluhu.
Arsenal leo wanasafiri hadi Bolton kucheza na Bolton mechi itakayoaanza saa 1 na nusu usiku bongo taimu.

No comments:

Powered By Blogger