Tuesday 16 September 2008


UEFA CHAMPIONS LEAGUE:


CHELSEA v BORDEAUX

saa 3 dak 45 usiku [bongo taimu]
Leo timu iliyobwagwa Fainali ya michuano hii msimu uliopita na Mabingwa Man U ikiongozwa na Meneja Mbrazil Luis Felipe Scolari, Chelsea, inashuka uwanjani kwake STAMFORD BRIDGE kupambana na timu ya Ufaransa Bordeaux ambayo inaongozwa na Meneja Laurent Blanc aliekuwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa iliyotwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 na vilevile tutamkumbuka kuwa aliwahi kuwa Beki wa Mabingwa Man U. [PICHANI NI LAURENT BLANC na SCOLARI wakicheka pamoja].
Mpaka leo Laurent Blanc ndie anaeshikilia rekodi ya kuwa Mchezaji 'mzee' aliefunga bao kwenye michuano hii ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE pale alipofunga goli wakati akichezea Man U kwenye mechi na Olympiakos Oktoba 2002. Alifunga goli hilo akiwa na miaka 36 na siku 339.
Leo Chelsea itamkosa Mfungaji wao stadi Didier Drogba ambae amefungiwa kucheza baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi ya Fainali ilipobwagwa na Man U huko Moscow mwezi Mei.

No comments:

Powered By Blogger