Tuesday 16 September 2008


UEFA CHAMPIONS LEAGUE:

MARSEILLE v LIVERPOOL

saa 3 dak 45 usiku [bongo taimu]

MECHI LAIVU DSTV SS3

Baada ya furaha ya kuishinda Man U Jumamosi kwa mabao 2-1, leo Liverpool wanatua nchini Ufaransa mjini Marseille kwenye uwanja uitwao STADE VELODROME kupambana na Timu ngumu ya Marseille kwenye mechi ya KUNDI D. Msimu ulioisha timu hizi zilikuwa Kundi moja na Marseille walimudu kuwatungua Waingereza hao bao 1-0 Uwanja wa Anfield ingawa nao walitwangwa mabao 4-0 kwenye uwanja huu wao wa nyumbani.
Leo Liverpool wanategemea kuwaanzisha nyota wao Nahodha Steven Gerrard na Mshambuliaji Fernando Torres.
Nao Marseille watakuwa tena na nyota wao ambao walikuwa majeruhi Mathieu Valbuena na Hatem Ben Arfa.
TIMU YA LIVERPOOL INATEGEMEWA KUWA:
Reina, Dossena, Arbeloa, Agger, Skrtel, Carragher, Gerrard, Alonso, Mascherano, Lucas, Benayoun, Babel, Kuyt, Torres, Riera, Keane, Cavalieri, Degen.

No comments:

Powered By Blogger