Tuesday 16 September 2008

TOTTENHAM 1 ASTON VILLA 2
Timu ya Tottenham ikicheza nyumbani uwanjani kwake White Hart Lane imepigwa bao 2-1 na Aston Villa jana usiku. Mpaka sasa Tottenham wamecheza mechi nne za LIGI KUU UINGEREZA na wameambulia pointi moja tu walipotoka suluhu ya bao 1-1 na Chelsea.
Aston Villa walipata bao la kwanza dakika ya nne tu ya mchezo baada ya krosi ya Gabriel Agbonlahor kumaliziwa kirahisi na Nigel Reo-Cocker. Goli la pili la Villa lilipatikana kwenye dakika ya 54 baada ya shuti dhaifu la Ashley Young kumpita kiajabu Kipa wa Tottenham Heurelho Gomes.
Darren Bent aliwapatia Tottenham kifuta machozi kwenye dakika ya 87.
Tottenham jana waliwachezesha kwa mara ya kwanza Wachezaji wao wapya Mshambuliaji wa Urusi Roman Pavlyuchenko na Beki wa Croatia Vedran Corluka.

No comments:

Powered By Blogger