Tuesday 16 September 2008


LEO USIKU UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUTIMUA VUMBI ULAYA!!

Mechi nane zinachezwa miji mbalimbali Ulaya leo usiku saa 3 dakika 45 saa za kibongo na zitakutanisha timu zenye matumaini tofauti.
Kwa sasa ukweli uliopo Ulaya ni kwamba timu za Uingereza ndizo zinazotawala Soka ya Klabu huko Ulaya na hili linadhihirishwa na kuweza kuingiza timu tatu kwenye Nusu Fainali ya michuano hii msimu uliokwisha na hatimaye kuingiza timu zao mbili Fainali huku Manchester United ikiibuka Bingwa.
Vilevile, kwenye tuzo ya Wachezaji Bora, Klabu hizo zilizoa tuzo zote kwani Ronaldo wa Man U aliibuka ndie Mchezaji na Mfungaji Bora, huku tuzo za Kipa, Mlinzi na Kiungo Bora zikienda kwa Wachezaji wa Chelsea ambao ni Petr Cech, John Terry na Frank Lampard.
Katika mechi za leo nane, Klabu za Uingereza zinazocheza ni Chelsea na Liverpool na mechi zao ni: Chelsea v Bordeaux na Marseille v Liverpool.
Timu nyingine Ulaya ambazo ni tishio na ambazo zipo uwanjani leo ni Barcelona, Inter Milan na AS Roma.
Timu ngeni kabisa ambazo zipo dimbani leo ni Anorthosis Famagusta ya Cyprus na timu ya Romanian CFR Cluj.
MECHI KAMILI NA MAKUNDI YA TIMU NI:
KUNDI A

CHELSEA v BORDEAUX

AS ROMA v CFR CLUJ

KUNDI B

PANATHINAIKOS v INTER MILAN

WERDER BREMEN v ANORTHOSIS FAMAGUSTA

KUNDI C

BARCELONA v SPORTING LISBON

BASEL v SHAKHTAR DONETSK

KUNDI D

MARSEILLE v LIVERPOOL

PSV EINDHOVEN v ATLETICO MADRID

No comments:

Powered By Blogger