Monday 15 September 2008

RONALDO KUONEKANA UWANJANI JUMATANO!!




Cristiano Ronaldo, Mchezaji Bora na Mfungaji Bora wa LIGI KUU UINGEREZA pamoja na LIGI YA MABINGWA YA ULAYA, atarudi tena uwanjani siku ya Jumatano wakati timu yake ambayo pia ni Mabingwa wa LIGI KUU UINGEREZA pamoja na ULAYA Manchester United itakapocheza na Villareal ya Spain kwenye michuano ya LIGI YA MABINGWA ULAYA Uwanjani Old Trafford.
Ronaldo alifanyiwa operesheni ya enka mwezi Julai na ilitegemewa atakuwa nje ya uwanja hadi mwezi Oktoba lakini sasa amepata nafuu haraka na Meneja Sir Alex Ferguson amethibitisha atacheza mechi hiyo.
Wakati Ronaldo akiwa nje ya uwanja alihusishwa sana na habari kwamba atahamia Real Madrid taarifa ambazo ziliwakera wapenzi wengi wa Man U.
Hata hivyo Ronaldo mwenyewe amesema haogopi jinsi washabiki watakavyompokea siku hiyo kwani yeye siku zote amekuwa akicheza kwa moyo mmoja na nguvu zake zote daima anapovaa jezi ya Man U.

No comments:

Powered By Blogger