Wednesday 17 September 2008

MAN U KUANZA KUTETEA TAJI LAO LEO!!!

==Arsenal wako Kiev ambako hawajahi kushinda!!!!

Manchester United, Mabingwa wa Ulaya, leo wanaanza utetezi wao wa Kombe la UEFA Champions League kwa kucheza nyumbani kwao Old Trafford na timu ngumu ya Spain Villarreal katika mechi ya KUNDI E na kujaribu kuweka historia ya kuwa Bingwa wa kwanza mtetezi wa Kombe la LIGI ya MABINGWA wa UEFA kumudu kutetea taji lake.
Tangu mfumo wa kutafuta Klabu Bingwa Ulaya ubadilishwe [pamoja na kubadilisha jina la michuano hii] kutoka mtindo wa mtoano na kuja mtindo wa ligi na kutoka jina la Kombe la Ulaya na sasa kuitwa LIGI ya MABINGWA wa UEFA hapo mwaka 1992, hakuna hata timu moja iliyonyakua kombe hili ikafanikiwa kulitetea msimu unaofuata mara baada ya kulinyakua.
Timu pekee iliyokaribia kuweka historia ni Klabu ya Juventus ya Italia ambayo ilinyakua Kombe la LIGI ya MABINGWA wa UEFA mwaka 1997 kwa kuifunga Borrusia Dortmund lakini wakakwama mwaka uliofuata walipopigwa kibao 1-0 na Real Madrid kwenye Fainali ya mwaka 1998.
Mechi nyingine kwenye kundi la Man U ni kati ya Aalborg ya Denmark na Celtic ya Scotland.
Katika kuanza utetezi wa taji lao Man U huenda wakaongezewa nguvu baada ya kujulikana Mchezaji na Mfungaji Bora Ulaya Cristiano Ronaldo amepona. Man U watawakosa Viungo Michael Carricl alievunjika mfupa mguuni siku ya Jumamosi kwenye mechi na Liverpool na Paul Scholes ambae amefungiwa mechi hii baada ya kula kadi nyekundu kwenye mechi ya Super Cup zidi ya Zenit St Petersburg.
Vilevile kuna hatihati ya Mchezaji mpya Dimitar Berbatov kucheza baada ya kupata maumivi ya goti kwenye gemu ya Jumamosi ya Liverpool na Meneja Sir Alex Ferguson amesema kama hachezi nafasi iko wazi kwa Manucho, Fowadi hatari wa Angola, kupewa namba.
TIMU ITATOKA KWA HAWA:
Van der Sar, Kuszczak, Foster, Brown, Neville, R Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evans, O'Shea, Evra, F Da Silva, Ronaldo, Nani, Hargreaves, Anderson, Possebon, Fletcher, Park, Giggs, Tevez, Rooney, Berbatov, Manucho, Welbeck.

Nao Arsenal ambao wako KUNDI G wanaanza kampeni yao leo kwa kuwatembelea Dynamo Kiev na historia inaonyesha hawajahi kushinda huko kwenye nchi za umoja wa zamani wa Kirusi hata siku moja!

Mwaka 1998 na 2003 walifungwa huko Kiev na 2006 walipigwa na CSKA Moscow wakati 2001 walibamizwa na Spartak Moscow.

Hata Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri: 'Mechi za huku ni ngumu sana! Tumepata matatizo huku kwani kila mara wanatushangaza kwa jinsi wanavyojitutumua na kujituma. Lakini safari hii tumeshajifunza!'

Mechi nyingine kwenye KUNDI G la Arsenal ni PORTO V FENERBAHCE.

No comments:

Powered By Blogger