Wednesday 6 May 2009

Arsenal wapata faraja kidogo-yanyakua Kombe la FA la Wanawake!!!!!!
Wakati msimu huu unaisha kwa mara nyingine tena Arsenal kutokuchukua Kombe lolote na mara ya mwisho kuchukua Kikombe ilikuwa 2005 walipotwaa FA CUP kwa kuitoa Manchester United kwa matuta, Klabu hiyo imepata faraja kubwa baada ya Timu yao ya Wanawake kuifunga Sunderland 2-1 na kutwaa Kombe la FA la Wanawake.

Hii ni mara ya 4 mfululizo kwa Timu hiyo ya Wanawake ya Arsenal kuchukua Kombe hilo.

Hao Arsenal Wanawake wanaweza pia kutwaa Kombe la LIGI KUU England kwa Wanawake wakiifunga Everton wiki ijayo.

No comments:

Powered By Blogger