Nani kuungana na Wolves na Birmingham kupanda Daraja kuingia LIGI KUU England?
Baada ya Wolverhampton Wanderers kushika nafasi ya kwanza na Birmingham nafasi ya pili kwenye Ligi ya Coca Cola Championship na hivyo kuingia moja kwa moja LIGI KUU England msimu ujao, Timu ya 3 itakayounga nao itatokana na mtoano maalum unaozishirikisha Timu 4 zilizoshika nafasi ya 3 hadi ya 6 na nazo ni Reading, Preston, Burnley na Sheffield United.
RATIBA YA MTOANO HUO NI:
-MEI 8, PRESTON V SHEFFIELD UNITED
-MEI 9, BURNLEY V READING
-MEI 11, SHEFFIELD UNITED V PRESTON
-MEI 12, READING V BURNLEY
Mshindi kati ya Preston v Sheffield United na Burnley v Reading watakutana Fainali huko Wembley na ataeibuka mshindi wa Fainali hiyo ndio anapandishwa Daraja.
BOSINGWA NA DROGBA WAOMBA MSAMAHA!! Barcelona wamsifia Nahodha wa Chelsea John Terry!!!
Baada ya kumvamia na kumtukana Refa Tom Henning Ovrebo kutoka Norway aliechezesha mechi ya juzi kati ya Chelsea na Barcelona iliyoisha sare ya 1-1 lakini Barcelona ametinga Fainali kwa goli la ugenini, Wachezaji wa Chelsea Jose Bosingwa na Didier Drogba waomba radhi kwa kauli na vitendo vyao.
UEFA inachunguza vitendo vya Chelsea pamoja na Ripoti ya Refa na imeahidi kutoa uamuzi wa hatua gani zitachukuliwa wiki ijayo.
Wakati huohuo, Meneja wa Barcelona, Pep Guardiola, amemsifia Nahodha wa Chelsea John Terry kuwa ni muungwana na ni mwanamichezo wa kweli kwa kitendo chake cha kwenda kwenye chumba cha kubadili jezi cha Barcelona na kuwapongeza huku akimpa mkono kila mtu ndani ya chumba wakiwemo Makocha na Wachezaji wote.
Kitendo hicho kilishangiliwa sana na Wachezaji wa Barcelona na wakaanza kumuimba wakimpongeza.
Pep Guardiola amesema: 'Natoa shukrani zangu za dhati kwa John Terry! Ni muungwana wa kweli!!'
UEFA CUP: FAINALI NI Werder Bremen v Shakhtar Donetsk!!!
Jana Werder Bremen iliibuka na ushindi wa ugenini wa 3-2 dhidi ya Wajerumani wenzao Hamburg na hivyo kutinga Fainali ya UEFA CUP.
Katika mechi ya kwanza Hamburg walishinda pia ugenini kwa bao 1-0 lakini Werder Bremen wameweza kusonga mbele kwa kufunga magoli mengi ugenini.
Sasa Werder Bremen watapambana Timu ya Ukraine Shakhtar Donetsk waliowabwaga wenzao wa Ukraine Dynamo Kiev kwa mabao 2-1.
Shakhtar Donetsk pia waliifunga Dynamo Kiev bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza.
Fainali ya Kombe hili ni 20 Mei 2009.
RATIBA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII: [saa ni za bongo]
Jumamosi, 9 Mei 2009
[saa 11 jioni]
Blackburn v Portsmouth
Bolton v Sunderland
Everton v Tottenham
Fulham v Aston Villa
Hull City v Stoke City
West Brom v Wigan
[saa 1 na nusu usiku]
West Ham v Liverpool
Jumapili. 10 Mei 2009
[saa 9 na nusu mchana]
Man U v Man City
[saa 12 jioni]
Arsenal v Chelsea
Jumatatu, 11 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Newcastle v Middlesbrough
Jumatano, 13 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Wigan v Man U [HII NDIO ILE MECHI YA KIPORO YA MAN U YA MUDA MREFU]
No comments:
Post a Comment