Monday 4 May 2009

Benitez ni kama 'Fisi' anaenyemelea mkono wa mtu udondoke!!!!
Baada hapo jana ya kuipiga 3-0 Timu 'dhaifu' iliyo kwenye hatari kubwa ya kushushwa Daraja, Newcastle, Rafa Benitez wa Liverpool bado anajipa matumaini makubwa ya kutwaa Ubingwa!!
Liverpool wamebakisha mechi 3 kumaliza Ligi na wana pointi 77 wakati Mabingwa Watetezi, Manchester United, wana pointi 80 huku wakiwa wamebakiwa na mechi 4.
Baada ya ushindi wa jana Benitez alikaririwa akisema: 'Jana tungefunga mabao mengi! ila nimewaambia Wachezaji waongeze bidii kwani Manchester akifanya makosa tuchukue Ubingwa. Manchester ni timu nzuri lakini naamini watafanya makosa na tutawapita!'
Ili Liverpool achukue Ubingwa, kwanza, lazima ashinde mechi zake zote 3 zilizobaki na, pili, aombe Manchester United wapoteze mechi 2 kati ya zao 4 zilizobaki!!!
Lakini Manchester United anaweza kutwaa tena Ubingwa, bila kujali Liverpool kafanya nini, akishinda mechi 2 na kupata sare 1 katika mechi zake 4 zilizobaki.
MECHI ZILIZOBAKI [Timu inayotajwa kwanza iko nyumbani]:
LIVERPOOL:
-Mei 9, West Ham v Liverpool
-Mei 17, West Brom v Liverpool
-Mei 24, Liverpool v Tottenham
MANCHESTER UNITED:
-Mei 10,Man U v Man City
-Mei 13,Wigan v Man U
-Mei 16, Man U v Arsenal
-Mei 24, Hull City v Man U

No comments:

Powered By Blogger