RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND:
Jumapili, 3 Mei 2009
[saa 9 na nusu mchana]
Liverpool v Newcastle
[saa 12 jioni]
Sunderland v Everton
Jumatatu, 4 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Aston Villa v Hull
NANI KUPANDA DARAJA KUINGIA LIGI KUU ENGLAND MSIMU UJAO?
LEO NDIO MWAMUZI!!!!!!
Ligi iitwayo COCA COLA CHAMPIONSHIP ikiwa ni Daraja la chini tu ya LIGU KUU England leo inafikia tamati na mbali ya Timu ya Wolverhampton Wanderers, maarufu kama Wolves, ambayo tayari imenyakua Ubingwa na hivyo kupanda daraja kuingia LIGI KUU, Timu za Birmingham, Sheffield United na Reading bado zina matumaini ya kuungana na Wolves kwani mojawapo ikipata matokeo mazuri leo pia itapandishwa.
Kawaida ni Timu 3 hupanda Daraja na 3 hushuka toka LIGI KUU. Timu mbili zinazopanda Daraja moja kwa moja ni ile Bingwa na ya pili ni ile inayomaliza nafasi ya pili. Timu zinazoshika nafasi ya 3 hadi ya 6 hucheza mtoano maalum kuamua ipi moja itakayopanda Daraja.
Mechi muhimu za leo zitakazoamua Timu moja ipi itashika nafasi ya pili na hivyo kuungana na Wolves kupanda Daraja moja kwa moja na kuingia LIGI KUU msimu ujao ni:
-Crystal Palace v Sheffield United
-Reading v Birmingham
Birmingham wakiwafunga Reading watapanda Daraja. Birmingham wakitoka suluhu wanaweza kupanda Daraja endapo tu Sheffield United hawashindi. Birmingham wakifungwa watakosa nafasi ya kupandishwa na wataingia kwenye mtoano maalum kuamua Timu ipi itashika nafasi ya 3 kupandishwa Daraja.
Sheffield United lazima washinde kwanza ili wawe na matumaini ya kushika nafasi ya pili na hivyo kupandishwa Daraja lakini hata hivyo hii itategemea matokeo ya mechi ya Reading v Birmingham.Ikiwa Sheffield United na Reading watashinda au Sheffield United watashinda na mechi ya Reading na Birmingham kuwa suluhu basi Sheffield United watapanda Daraja.
Reading pia lazima washinde na kuomba Sheffield United isishinde ili wapandishwe. Endapo Reading atashinda na Crystal Palace watatoka suluhu na Sheffield United Timu zote 3 yaani Reading, Birmingham na Sheffield United zitakuwa na pointi sawa, pointi 80, lakini Reading atapandishwa kwa kuwa na tofauti ya magoli bora.
Timu mbili kati ya Birmingham, Sheffield United na Reading ambazo zitakwama kupanda Daraja zitaingia moja kwa moja kwenye mtoano maalum wa Timu 4 kuamua ipi moja itaungana na Bingwa Wolves na Timu itakayoshika nafasi ya pili kupanda Daraja.
Timu nyingine 2 zitakazoingia kwenye mtoano huo maalum zitatokana na Timu za Cardiff, Burnley na Preston.
Hivyo, kwa kifupi, Wolverhamton Wanderers ashapanda Daraja na Timu mbili nyingine zitakazoungana nae kuingia LIGI KUU msimu ujao zitatoka kati ya Birmingham, Sheffield United, Reading, Cardiff, Burnley na Preston.
No comments:
Post a Comment