Middlesbrough 0-2 Man Utd
Manchester United polepole wananyemelea kutetea Ubingwa wao wa LIGI KUU England baada ya jana kushinda ugenini Riverside Stadium walipoifunga Middlesbrough, timu iliyo hatarini kuteremshwa daraja, mabao 2-0. Huku wakichezesha Kikosi kilichobadilika na kile kilichoifunga Arsenal ba0 1-0 siku ya Jumatano kwenye mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Man U wakiongozwa na wakongwe wao Ryan Giggs na Paul Scholes waliandika bao la kwanza mfungaji Giggs dakika ya 25.
Kipindi cha pili mnamo dakika ya 52 Ji-Sung Park akafunga bao la pili kufuatia pasi murua ya Wayne Rooney.
Kwa ushindi huo, Man U sasa wana pointi 80 kwa mechi 34 wakiwa mbele ya Liverpool kwa pointi 6 ambao wana pointi 74 kwa mechi 34.
Leo jioni Liverpool wanaivaa Newcastle kwake Anfiled.
Lakini balaa kubwa lipo kwa Middlesbrough kwani wamebakisha mechi tatu tu na wako nafasi ya 19 huku wakiwa na pointi 31 sawa na Newcastle walio nafasi ya 18 huku West Bromwich iko nafasi ya 20 ambayo ni ya mwisho na wana pointi 28.
Timu zilizo nafasi ya 18, 19 na 20 hushushwa Daraja.
Middlesbrough: Jones, McMahon (Digard 55), Wheater, Huth, Hoyte, O'Neil (Emnes 70), Sanli, Bates, Downing, King (Alves 55), Aliadiere.
Akiba hawakucheza: Turnbull, Arca, Adam Johnson, Grounds.
Kadi: Huth.
Man Utd: Foster, O'Shea, Vidic, Evans, Evra (Rafael Da Silva 78), Park (Nani 74), Scholes, Giggs, Rooney, Berbatov, Macheda (Tevez 55).
Akiba hawakucheza: Kuszczak, Ronaldo, Anderson, Gibson.
Kadi: Macheda.
Watazamaji: 33,767
Refa: Mark Halsey
Chelsea 3-1 Fulham
Chelsea walianza mechi hii wakiwa kwao Stamford Bridge kwa moto mkubwa sana na iliwachukua sekunde 51 tu kuchomeka bao la kwanza lililoingizwa na Nikolas Anelka na Fulham wasawazisha dakikatu baadae mfungaji akiwa Erik Nevland.
Lakini kwenye dakika ya 10, Malouda akawapeleka mbele kwa kufunga bao la pili na Didier Drogba akaweka la 3 kipindi cha pili.
Sasa Chelsea wamebakisha mechi 3 na wako nafasi ya 3 nyuma ya Liverpool.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Alex (Ivanovic 46), Terry, Ashley Cole, Lampard, Essien (Ballack 46), Mikel, Malouda, Anelka, Drogba (Di Santo 84).
Akiba hawakucheza: Hilario, Kalou, Belletti, Mancienne.
Fulham: Schwarzer, Pantsil, Hughes, Hangeland, Konchesky, Dempsey, Etuhu, Murphy, Gera, Zamora (Dacourt 76), Nevland (Kamara 35).
Akiba hawakucheza: Zuberbuhler, Gray, Stoor, Baird, Smalling.
Kadi: Murphy.
Watazamaji: 41,801.
Refa: Alan Wiley , Arsenal
Portsmouth 0-3 Arsenal
Kwa ushind huu, Arsenal wamejihakikishia angalau nafasi ya 4 kwenye ligi na hivyo kuwa na uhakika wa kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao kwani timu inayowafukuza Aston Villa walio nafasi ya 5 sasa wamepitwa pointi 13 na wamebakisha mechi 4 tu.
Arsenal walifanya mabadiliko ya Kikosi huku wakipumzisha Wachezaji wa nane waliocheza Jumatano iliyopita na Man U lakini hilo halikuwazuia kutawala mechi hii ya ugenini na ushindi huo wa jana umewafanya sasa wawe wamecheza mechi 21 za ligi bila kufungwa.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Bendtner dakika ya 13 na 41 [kwa penalt]na Vela dakika ya 56. Portsmouth: James, Pamarot, Campbell, Distin, Hreidarsson (Kanu 46), Pennant (Utaka 46), Davis, Hughes, Mullins, Belhadj, Crouch.
Akiba hawakucheza: Begovic, Primus, Nugent, Basinas, Cranie.
Kadi Nyekundi: Pamarot (dakika ya 78).
Kadi: Campbell, Kanu, Davis.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Song Billong, Djourou, Eboue, Walcott (Bischoff 64), Denilson, Ramsey (Randall 82), Arshavin, Bendtner (Merida 77), Vela.
Akiba hawakucheza: Mannone, Coquelin, Emmanuel-Thomas, Frimpong.
Kadi: Arshavin.
Watazamaji: 20,418
Refa: Lee Mason
MATOKEO MECHI NYINGINE ZA LIGI KUU:
Tottenham 1 West Brom 0
Man City 3 Blackburn 1
Stoke 0 West Ham 1
Wigan 0 Bolton 0
'EL CLASICO': Barcelona waibomoa Real Madrid nyumbani kwake!!!!!
Hizo ni salaam maalum kwa Chelsea!!!!
Barcelona, wakicheza ugenini Santiago Berbabeu uwanjani kwa Real Madrid, jana usiku waliwafumua watani zao wa jadi kwa mabao 6-2 na sasa kuongoza ligi wakiwa mbele kwa pointi 7.
Pengine hizi ni salaam maalum kwa Chelsea kwani baada ya kutoka suluhu 0-0 huko Nou Camp kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, sasa Barcelona watatua Stamford Bridge Jumatano kurudiana na Chelsea.
Real ndio walianza kufunga bao la kwanza kupitia kwa Gonzalo Higuain na Barcelona wakasawazisha kupitia kwa Thierry Henry na Puyol na Lionel Messi wakaongeza kuwafanya Barcelona wawe mbele 3-1.
Sergio Ramos akaifungia Real bao la pili lakini mvua ya Magoli iliendelea kuporomoshwa kupitia Thierry Henry, bao la 4, Lionel Messi la 5 na Mchezaji wa zamani wa Man U, Gerrard Pique, akafunga kitabu kwa bao la 6.
No comments:
Post a Comment