Saturday 9 May 2009

Stoke City wajinusuru, wabaki LIGI KUU!!!!!!!

Stoke City wakicheza ugenini KC Stadium wamewafunga wenyeji wao Hull City mabao 2-1 na kufikisha pointi 42 ambazo zimewahakikishia kubaki LIGI KUU msimu ujao huku wakiwa wamebakisha mechi 2 ligi kufikia tamati. Kwa kipigo hiki, Hull City mpaka sasa hawajui hatima yao huku wakiwa na pointi 34 na wamebakisha mechi 2 tu, moja watacheza na Bolton ugenini na ya mwisho watakuwa nyumbani kupambana na Mabingwa Watetezi wa ligi hiyo Manchester United.
Hull wako nafasi ya 17 wakifuatiwa na Timu zilizo nafasi ya kuporomoka Daraja yaani nafasi ya 18 ni Newcastle pointi 31, nafasi ya 19 ni Middlesbrough pointi 31 na wa mwisho ni West Bromwich pointi 31 na yuko nafasi ya 20.
Newcastle na Middlesbrough, waliocheza mechi moja pungufu ya Hull City, wanacheza pamoja Jumatatu usiku na ikiwa Newcastle atashinda basi atakuwa na pointi 34 sawa na Hull City lakini Hull atashushwa hadi nafasi ya 18 kwa kuwa ana uhafifu wa magoli na hilo ni eneo hatari la kuporomoka Daraja.
Timu iliyo mkiani yashinda!!!! Je yaweza kujinusuru kuteremshwa Daraja?
West Brom 3 Wigan 1
West Bromwich Albion, Timu ambayo iko mkiani mwa LIGI KUU kwa muda mrefu sasa, leo imeweza kuifunga Wigan, Timu iliyo nafasi ya 11, kwa mabao 3-1 na hivyo kufikisha pointi sawa na Timu mbili zilizo juu yake, yaani Middlesbrough na Newcastle, zote zikiwa na pointi 31 lakini wanatenganishwa kwa tofauti ya magoli.
Timu hizi 3, Newcastle, Middlesbrough na West Brom, zote zipo nafasi za mwisho na kimsimamo Timu zinazokuwa nafasi hizo hushushwa Daraja mwishoni mwa ligi.
Juu ya Timu hizi ipo Hull City wenye pointi 34 lakini Newcastle na Middlesbrough, waliocheza mechi moja pungufu ya Hull City, wanacheza pamoja Jumatatu usiku na ikiwa Newcastle atashinda basi atakuwa na pointi 34 sawa na Hull City lakini Hull atashushwa hadi nafasi ya 18 kwa kuwa ana uhafifu wa magoli na hilo ni eneo hatari la kuporomoka Daraja.
West Bromwich wamebakisha mechi mbili moja wanacheza nyumbani na Liverpool na ya mwisho ugenini na Blackburn.
Blackburn 2 Portsmouth 0
Blackburn polepole wanaanza kujinasua toka balaa la kushushwa Daraja baada ya leo kuwapiga Portsmouth 2-0 na hivyo kufikisha pointi 40 na kuwaacha Portsmouth wakiwa na pointi 38.
Ingawa bado kimahesabu Blackburn hajanusurika lakini ushindi huu unawapa afueni kubwa hasa ukizingatia ukweli kuwa Timu tatu za mwisho ni Newcastle, Middlesbrough na West Brom , ambazo ziko hatarini kuporomoshwa Daraja zina pointi sawa, pointi 31, na kizuri zaidi ni kuwa Newcastle na Middlesbrough wanapambana wenyewe Jumatatu usiku.
MATOKEO KAMILI MECHI ZILIZOCHEZWA JUMAMOSI MEI 9 KUANZIA SAA 11 JIONI [Bongo taimu}
Blackburn 2-0 Portsmouth
Bolton 0-0 Sunderland
Everton 0-0 Tottenham
Fulham 3-1 Aston Villa
Hull City 1-2 Stoke City
West Brom 3-1 Wigan

No comments:

Powered By Blogger