Tuesday 5 May 2009

LEO NA KESHO MACHO YA DUNIA YAKO LONDON: MARUDIO NUSU FAINALI KUCHEZWA HUKO!!!!!!
Leo na kesho mji wa London utawaka moto kwani zile mechi za marudio za UEFA CHAMPIONS LEAGUE zitachezwa na leo ikiwa Uwanja wa Emirates, ambako Timu za England pekee zinakutana, wakati wenyeji Arsenal wataikaribisha Manchester United ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili.

Kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa nyumbani kwa Man U Old Trafford, Man U walishinda bao 1-0 na hivyo Arsenal lazima ashinde 2-0 ili aingie Fainali. Endapo Arsenal wataruhusu Man U wapate bao moja basi itabidi wafunge bao 3 ili washinde.

Kesho ni zamu ya Stamford Bridge wakati wenyeji Chelsea wanarudiana na Barcelona baada ya kutoka dro mechi ya kwanza kwa bao 0-0 na hivyo Chelsea lazima ashinde ili asonge mbele kwani suluhu ya magoli ya aina yeyote ile itawapa ushindi Barcelona kwa vile wako ugenini na magoli ya ugenini huhesabika mawili endapo timu zinatoka suluhu.

Hata hivyo inabidi Chelsea waingie kwa tahadhari kubwa kwani Barcelona wakicheza ugenini tena nyumbani kwa Watani zao wa jadi, Real Madrid siku ya Jumamosi, waliifumua Real mabao 6-2!!

LIGI KUU ENGLAND: Hull City wazidi kudidimizwa!!!!

Jana usiku, Aston Villa wameifunga Hull City bao 1-0 kwa bao la John Carew uwanjani Villa Park na kuzidi kuwapa wasiwasi Hull wa kukumbwa na balaa la kushushwa Daraja kwani wako nafasi ya 17 na wako juu tu ya Timu 3 za chini za mwisho ambazo huteremshwa Daraja kwa pointi 3 tu.
Timu 3 za mwisho ni ile ya nafasi ya 18 inayoshikiliwa na Newcastle wakiwa na pointi 31 sawa na Timu ya 18 Middlesbrough.
Mkiani wapo West Brom wenye pointi 28.
Mechi zilizobaki Ligi kwisha ni 3.

No comments:

Powered By Blogger