Wednesday 6 May 2009

Baada ya Mechi=Kauli za Ferguson na Wenger!!

Baada ya kindumbwendumbwe cha jana cha Emirates Stadium ambapo Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Manchester United, waliwatoa nishai wenyeji wao Arsenal kwa kuwapiga bao 3-1 ukiwa ni ushindi wao wa pili baada ya kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza huko Old Trafford na hivyo kutinga Fainali huko Rome hapo Mei 27 kupambana na mshindi wa leo kati ya Chelsea v Barcelona, Mameneja wa Timu zote mbili walizungumzia pambano.
FERGUSON:

-Walishindwa kumdhibiti Ronaldo-yeye ndio tofauti ya mechi hii!!!!
-Magoli mawili ya haraka yaliwatoa upepo!!
-Wenger anastahili sifa kwani anafanya kazi kwa bidii na uadilifu. Tatizo kwa Wenger na mimi ni kuwa kadri unavyozidi kudumu kwenye soka unapachikwa lebo nyingi tu! Ushinde au ufungwe. Ukifungwa, we ni bure tu hufai, ukishinda, we ndo kidume tu!!!
WENGER:

-Ni usiku mbaya sana kwenye maisha yangu ya soka!!
-Mashabiki walitegemea usiku mkubwa kwao. Tumewaangusha, inauma sana!!!
-Kitu kigumu ni kuwa hatujisikii kama tulicheza Nusu Fainali ya Ulaya!! Tulitolewa baada ya dakika 10 tu!!
-Hatumlaumu mtu binafsi!! Ndani ya dakika 3 tumepigwa bao 2 na hilo ni balaa kubwa!!
-Nahitaji kukaa mbali na msimu huu!! Tulicheza mechi 21 bila kufungwa lakini katika mechi kubwa na Chelsea na Man U hatukushinda na hilo linahitaji kulifikiri!!
-Lakini, tumefungwa na Man U timu inayofanya kuua ni kama sanaa na ukifanya kosa tu wanakumaliza!! Na Ronaldo alitupa wakati mgumu sana!!!

No comments:

Powered By Blogger