Ni Wanaume Manchester United v Barcelona huko Rome Mei 27!!!!
Chelsea, wakiwa kwao Stamford Bridge, wamekatwa maini dakika ya mwisho baada ya Andres Iniesta wa Barcelona kusawazisha bao dakika ya 90 na kufanya mechi iwe 1-1 na hivyo Barcelona kuingia Fainali kwa goli la ugenini. Mechi ya kwanza kati yao huko Nou Camp, Barcelona ilimalizika 0-0.
Chelsea walipata bao la kuongoza kipindi cha kwanza dakika ya 8 tu baada ya mpira uliopigwa na Frank Lampard kuelekea ndani ya boksi kumbabatiza Yaya Toure na kupaa juu na kumkuta Michael Essien alieachia kigongo kilichogonga besera juu na kushuka ndani ya wavu.
Eric Abidal wa Barcelona alipewa Kadi Nyekundu na Refa kutoka Norway Tom Henning Ovrebo kwa kumchezea rafu Anelka na hivyo atakosa kucheza Fainali.
Katika mechi hii, mara kadhaa Refa alionekana akiwaminya Chelsea penalti kadhaa.
Kwa matokeo haya, Fainali Rome, Italy ndani ya Olympic Stadium tarehe 27 Mei 2009 ni kati ya Mabingwa Watetezi Manchester United na Barcelona.
No comments:
Post a Comment