Friday 22 May 2009

UEFA YAFUNGUA MASHTAKA KWA CHELSEA NA WACHEZAJI DROGBA NA BOSINGWA!!
  • JUNI 17 NDIO HUKUMU YAO!!!!
    UEFA, Chama cha Soka Ulaya, kimeifungulia Chelsea na Wachezaji wake Didier Drogba na Jose Bosingwa mashitaka kufuatia utovu wa nidhamu ulioonyeshwa mara baada ya mechi ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE iliyofanyika Stamford Bridge kati ya Chelsea na Barcelona matokeo yakiwa 1-1 lakini Barcelona akaingia Fainali kwa goli la ugenini.
    Chelsea kama Klabu imeshitakiwa kwa kosa la utovu wa nidhamu wa Wachezaji wake na kwa washabiki wake kutupa vitu uwanjani.
    Wachezaji Didier Drogba na Jose Bosingwa wameshitakiwa kwa kumkashifu Refa Tom Henning Ovrebo kutoka Norway.
    Washtakiwa wote wanatakiwa wajibu tuhuma hizo ifikapo 29 Mei 2009 na UEFA itatoa uamuzi Juni 17.

No comments:

Powered By Blogger